"Kutoa radhi" ni msemo ambao kwa kweli unabeba maana nzito sana ktk jamii nyingi za Kiafrika. Ktk imani za kijadi, wazazi ni kiungo baina ya nguvu za juu zilizo karibu na Mwenyezi Mungu na waja wake. Nguvu hizo huonekana zaidi pale wazazi wanapotangulia kuungana na wahenga wetu. Wakiwa huko wanaweza zaidi kuingia katika maisha ya wanao ambao bado wapo hapa duniani. Huko waliko wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Kwa hakika makabila mengine huwaita wahenga hao "malaika." Ili mzazi aliyetangulia aweze kukusaidia katika maisha yako ya hapa duniani, ni lazima anapoondoka awe amekuwa radhi nawe unayebaki. Akitoa radhi hiyo, basi huna msaada wake. Utahangaika mwenyewe tu. Na pengine anaweza si kuondoa radhi tu, bali pia akakuachia laana. Jambo hili ni baya zaidi. Mtazamo huu wa maisha husisitizwa sana kwa watoto kwa masimulizi ya watu mbalimbali na walivyokosa radhi na matokeo mabaya katika maisha yao. Mifano hai kama hiyo ina nguvu sana katika maisha yetu ya awali.
"Kumwaga radhi" ilianza kama namna moja ya kupindisha dhana hiyo kwa kujifurahisha na kuchekesha wasemaji wa Kiswahili. Na ilianza kwa namna ya kuelezea jambo ambalo mtu akilifanya ni aibu au kashfa fulani. Ni kana kwamba anafanya mambo ambayo yumkini yanawaudhi wahenga. Maana yake kwa sasa ni tofauti kabisa.
...ni kumlaani/kumtakia mabaya binadamu mwenzio kwa njia ya maneno au matendo (unavua c*h&&&&u@pi) kutokana na jambo baya alilolitenda machoni pa mtendwaji...watoa radhi wengi huwa ni wazazi/babu/bibi
Note : Radhi, Ridhi, Ridhia, Ridhiko, Ridhiana, Kumradhi, na yafananayo na hayo!
Hutokea pale maneno hayo yanapokua kinyume chake!
Aidha radhi si lazima itolewe na mzazi, ipo radhi ya mke kwa mumewe na ya mume kwa mkewe.