Nini maana ya Lila na fila hazitangamani

Nini maana ya Lila na fila hazitangamani

Utangamano ni Kama upatano, ushirikiano, upatano.

Wanaposema Lila na fila havitangamani humanisha ubaya na wema havipatani.
 
Kutangamana= kukaa pamoja/kupatana

Lila na fila ni maneno ya kibantu

Lila= lile
Fila = vile

Kwahiyo kwa Kiswahili cha kawaida inaweza kusomeka "Lile na Vile havikai pamoja"

Lila ikiwakilisha mtu mbaya/aliyetengwa (eg.lile lijamaa)

Fila ikiwakilisha watu wengine wazuri (wao)

Kwahiyo maana ya "Lila na fila havitangamani" inaweza kuwa

1. Wabaya na wazuri hawakai pamoja

2. Vibaya na vizuri havishabihiani
 
Back
Top Bottom