NINI maana ya MAGATUZI

NINI maana ya MAGATUZI

Shembago

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
332
Reaction score
50
Wana JF naomba mnisaidie huwa naangalia KBC TV na katika taarifa zao wanakipindi wanakiita Taarifa za Magatuzi,Nimejaribu kufuatilia ili hata nibahatishe lakini sipati picha.Nini maana ya Magatuzi?

Nawakilisha,
 
sina hakika na hilo neno ulilolisema, ila tuzungumzie UGATUZI, ni mgawanyo wa madaraka kutoka ule mfumo wa kitaifa, yaani serikali kuu kuwa na maamuzi yote, hadi mfumo wa kimajimbo, yaani serikali za majimbo kuwa na mamlaka zaidi ya kuamua mambo katika eneo lao. by the way hilo neno hutumika sana kwenye kiswahili cha huko jamhuri ya kenya.
 
hata mie huwa naangalia taarifa zao za habari hilo neno huwa ni geni sana kwangu
 
kenya imegawanyika katika majimbo arobaini na saba yaani majimbo hivyo wakisema ''habari za magatuzi'' maana yake ni habari za majimbo au habari toka majimboni. I stand to be corrected
 
kenya imegawanyika katika majimbo arobaini na saba yaani majimbo hivyo wakisema ''habari za magatuzi'' maana yake ni habari za majimbo au habari toka majimboni. I stand to be corrected

Nashangaa Tom huna LIKE hata moja? chukua hiyo hapo
 
Naamini mnaongelea DECENTRALIZATION katika baadhi ya maamuzi serikalini!
-Kumbuka Madaraka Mikoani enzi za Mwalimu.
 
Wanamaanisha taarifa toka twitter, face book etc
 
Back
Top Bottom