JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ni taasisi ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Uchumi iliyoanzishwa na Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya mwaka 1994 ili kusimamia na kuendeleza masoko ya mitaji hapa Tanzania.
Majukumu makubwa ya mamlaka hiyo ni pamoja na:-
a) Kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji Tanzania;
b) kuidhinisha uanzishwaji wa masoko ya hisa na mifuko ya uwekezaji wa pamoja, na kutoa leseni kwa wataalam wa masoko ikiwa ni pamoja na madalali, wachuuzi, wawakilishi wao, washauri wa uwekezaji, n.k.
c) Kusimamia masoko ya mitaji pamoja na wataalam wote wanaohusika na utendaji wa masoko hayo; na
d) Kuishauri Serikali kwenye masuala yote yahusuyo masoko ya mitaji na dhamana
Upvote
0