kuna msemo usemao
"Mchamaago hanyele huenda akwiya tena"
Msemo huu wa kiswahili unatumika tokaenzi ya mababu namababu lakini wengi wetu hatujui maana ya maneno yaliyotumika. Nawaombeni wakuu mtueleze maana ya maneno yafuataya:
Mchamaago,
Hanyele,
Akawiya.
Naomba kila neno litungiwe sentensi ili tujue vipi kulitumia.
Mimi ninvyojua ni "Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo".
Mchama ago (msafiri aliyeweka kambi mahala fulani katika safari yake) hanyeli (hanyi hapo kambini kwa sababu anaondoka - i.e. hafanyi mabaya) huenda (kuna uwezekano) akauya (akarudi) papo (hapo hapo kwenye kambi aliyoweka mwanzo).
Asante mkuu kwa ufafanuzi wako.Wengine husema MCHAMAAGO HANYELE HWENDA AKAWIA PAPO..............maana : anaehama /anaendoka sehemu asitukane (kufanya mambo mabaya) pengine atarudi tena papo hapo
Asante mkuu SMU.umetufafanulia vizuri sana.Mimi ninvyojua ni "Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo".Mchama ago (msafiri aliyeweka kambi mahala fulani katika safari yake) hanyeli (hanyi hapo kambini kwa sababu anaondoka - i.e. hafanyi mabaya) huenda (kuna uwezekano) akauya (akarudi) papo (hapo hapo kwenye kambi aliyoweka mwanzo).
Mimi ninvyojua ni "Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo".
Mchama ago (msafiri aliyeweka kambi mahala fulani katika safari yake) hanyeli (hanyi hapo kambini kwa sababu anaondoka - i.e. hafanyi mabaya) huenda (kuna uwezekano) akauya (akarudi) papo (hapo hapo kwenye kambi aliyoweka mwanzo).
Mimi ninvyojua ni "Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo".Mchama ago (msafiri aliyeweka kambi mahala fulani katika safari yake) hanyeli (hanyi hapo kambini kwa sababu anaondoka - i.e. hafanyi mabaya) huenda (kuna uwezekano) akauya (akarudi) papo (hapo hapo kwenye kambi aliyoweka mwanzo).
wapendwa,
hii methali nimewahi kuifafanua kwenye thread fulani. ufafanuzi wa SMU ni sahihi kabisa, ila naomba nifafanue vizuri zaidi hapo kwenye wino mwekundu.
kuchamaa =
kuchuchumaaago= mahali pafinyu (mfano pangoni ama chini ya mti mkubwa ulioinama) ambapo huwezi kusimama wima ama kujibanza ila kwa kuchuchumaa tu. mfano wa mtu aliyekumbwa na mvua kubwa akiwa porini aweza kukimbilia kwenye kapango kadogo kaliko karibu uli kujibanzxza pale na kujihifadfhi dhidi ya mvua hiyo kubwa.
sasa huyu aliyejibanza hapo pangoni kwa kujikunyata ama kuchuchumaa tu kutokana na ufinyu wa nafasi hapo pangoni, iwe ni kwa kujikinga na mvua, jua, baridi , wanyama wakali ama kulala wakati wa usiku nk, ndiye anayeitwa mchamaa ago! na ndiye tunayeambiwa hawezi kunya hapo maana huenda siku moja akapatwa na dharura nyingine na kujikuta akirudi kujihifadhi palepale.
mbarikiwe sana wapendwa.
Glory to God!