Nini Maana ya 'Mind' kwa Kiswahili (Kwa neno moja)

Nini Maana ya 'Mind' kwa Kiswahili (Kwa neno moja)

Inategemea na context, lakini kwa ujumla 'akili' ni sahihi.

He has lost his mind. = Amepoteza akili.

He has got a good mind. = Anayo akili nzuri.

Our mind is very important. = Akili yetu ni muhimu sana.

Use your mind! = Tumie akili yako!

---------

You have to tell me! I can't read your mind! = Lazima uniambie! Siwezi kutambua unafikirije! / Siwezi kutambua mawazo yako!

---------

I don't mind. = Kwangu ni haidhuru. / Ni mmoja tu. / Ni sawa.

--------

Mind how you go! = Nenda kwa uangalifu! / Nenda kwa utaratibu! Mind! = Angalie!

Haya kwa ufupi tu! Yapo expressions mengi!
 
Inaweza kuwa "mtazamo"
Mind set = mtazamo uliojengeka akilini.
 
ndo tabia ya watu wa JF jibu sahihi ni "FIKRA "
LAKINI MTU ATAENDLEA KUTAFUTA MAJIBU YALIYOKOSEA ILI KUYAKOSOA BADALA YA KUSITISHA MJADALA KWA KUKUBALI LILOSAHIHI
 
Mind ina maana zaidi ya moja na huwezi kuitafsiri kwa neno moja kama unavyoka
Labda utoe sentensi yenye neno mind kisha utake kujua inamaana gani kwenye hiyo sentense
 
ndo tabia ya watu wa JF jibu sahihi ni "FIKRA "
LAKINI MTU ATAENDLEA KUTAFUTA MAJIBU YALIYOKOSEA ILI KUYAKOSOA BADALA YA KUSITISHA MJADALA KWA KUKUBALI LILOSAHIHI

Hebu nisaidie kutafsiri hizi sentensi kama neno fikra lina fit mkuu
never mind the opinion polls
do you mind if I have a cigarette?
 
Usitake kutafsri direct msamiati wa lugha moja kwnda lugha nyingine . Lugha ya kiingereza ni lugha iliyotokana na lugha nyinge kama sikose ina baadhi ya misamiati ya kireno ..

Na kiswahili ina misamiati na taratibu za lugha ya kiharabu ..

Sasa ukitaka kutamfisiri maneno direct hutaweza kwani itakulazimu kuunga lugha karibia nne ambapo hutatoka na jibu sahihi ..
So yakupaswa kuchukua msamiati ulio karibu angalau kodogo na maana sahihi ya msamiati oanishi
 
Hebu nisaidie kutafsiri hizi sentensi kama neno fikra lina fit mkuu
never mind the opinion polls
do you mind if I have a cigarette?

Never mind the opinion polls. = Usijali kura za maoni.

Kwa ujumla 'Never mind' ina maana 'Haidhuru'

Do you mind if I have a cigarette? = Je, unijalie nivute sigareti? / Je, naweza kuvata sigareti? / Je, itakusumbua kama nikivuta sigareti?

Kwa ujumla 'Do you mind if I..' ina maana 'Je, unijalie ...' au 'Je, itakusumbua kama ...'

Pia angalie sentensi hapo juu kwenye post yangu ya kwanza.
 
mandella;

Kwa kweli kazi ya kutafsiri siyo jambo la kutafsiri neno moja moja directly katika sentensi. Kwa ujumla ukifanya hivyo utaharibu maana ya sentensi. Na hiyo ndiyo shida ya kutafsiri sentensi kwenye internet. Software haitambui maana ya sentensi – kwa ujumla inaweza kutafsiri maana ya neno moja tu (lakini hiyo inategemea na lugha).

Kazi ya kutafsiri ni kutafsiri maana ya sentensi nzima. Sasa ukijua lugha zote wawili (ya Kiswahili na ya Kiingereza) vizuri, unaweza kutafsiri maana ya sentensi.

Kwa hiyo angalie post zangu mbili hapo juu. (Sasa, Kiswahili changu siyo sahihi kabisa lakini nafikiri nilitoa maana ya Kiingereza kwenda Kiswahili kadiri watu wanavyoweza kuelewa?).
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sio kila neno la kiingereza linaweza kutafsiriwa moja kwa moja kuja kwenye kiswahili.
 
Mind: Jihadhari, kuwa mwangalifu, sehemu ya ubongo ya kutafakari, ''Je unajali nikivuta bangi tukiwa pamoja?''
 
Bila Kujali Maana Ya Sentens Yenye Muunganiko Wa Maneno Mengine,a Single Wrd MIND Ni Fikra,

Ikiwa N Sentes Bas Utailewa Kadri Ya Sentens Ilivo,
 
Back
Top Bottom