Nini maana ya mtu kuwa na gubu?

Nini maana ya mtu kuwa na gubu?

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
942
Reaction score
168
Kuna msemo watu huwa wanasema mtu huyu au yule ana gubu au chama fulani wafuasi wake wanagubu sielewi neno gubu linaashiria nini mwenye kuelewa atiririke hapa tujue.

Kuna mzee mmoja aliniambia atanieleza akipata nafasi kwa wakati huu anapilika za xmas.
 
Inaonekana ww unashambuliwa sana na watu kuwa una gubu, ngoja ipite Xmas huyo mzee akukalishe chini akuweke jando uache hilo gubu.
 
Hashuo,wahka,maudhi,hujielewi some time yes sometime no, unamarereeeee
 
gubu ni hali ya kumind vitu vidogovodogo na kuvikuza vionekane vikubwa katika hali ya ushari,mtu mwenye gubu hata ukimkwaa bahati mbaya atapiga kelele mtaa mzima ujue kuwa umemkanyaga hata ukimuomba samahani
 
Mtu aliye na gubu ni yule ambaye jambo lolote hata km ni dogo kiasi gani atalishikia bango ila kwa style ya manunguniko ya chini kwa chini ambayo siyo ya wazi. Na halitaisha mpk miezi ipite kila siku linakumbushiwa hilohilo. Usoni sura yake haioneshi hasira wala kisirani ila muda wote vimaneno vya hapa na pale.

Mwanamke usiombe kuolewa na mwanaume mweny gubu. Nje anacheka muda wote lkn mkishafika wenyewe ndani vimaneno lazima ukauke kama ukuni.
 
Mimi mwenyewe ni mzee wa gubu,kitu kidogo tu lazima nikumind [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom