Nini maana ya neno Muda

John Nash Jr

Member
Joined
Sep 13, 2018
Posts
54
Reaction score
59
Asalaam wakuu

Kumekuwa na mitazamo mingi na ukinzani wa fikra juu ya neno muda. Hadi sasa hakuna tafsiri wala maana moja inayoelezea neno muda ambayo imekubalika kwa wanazuoni wote.

Baadhi wanasema muda ni kipindi ambacho jambo fulani linafanyika na kujenga historia fulani ya kipekee ambacho hakijirudii kamwe. Wengine wanasema muda hauna kipimo maalum bali ni mfululizo tu wa matukio ambayo hutengeneza nyakati tofauti ili kutofautisha tukio moja na jingine.

Nataka kujua mtazamo wenu wakuu juu ya maana ya neno muda? Pia kuna uwezekano wa kuahirisha muda, vipi kuhusu uwezekano wa kwenda/kusafiri mbele au nyuma ya muda? Au muda ni fumbo tu ambalo binadamu tumefumbwa na hatulijui maana yake!

Nawasilisha
 
Huwezi kuahirisha muda,mfano hii sentensi, "tumeahirisha mpaka muda/wakati mwingine" muda ni kitu kinachokwenda mbele tu na kamwe hakirudi nyuma,jaribu kutizama saa yako ya mkononi au ya ukutani,jinsi ule mshale unavyokwenda ndio na muda unavyokwenda.
 
Mwanafizikia maarufu wa karne ya 20, Albert Einstein alipata kutoa ufanunuzi wa muda/wakati na alisema "muda ni "ile hali inayozuia matukio kutokea kipindi kimoja".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…