Nini maana ya ugatuzi

mzenjiboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
907
Reaction score
385
Hili neno 'ugatuzi' huwa nalisikia sana kwenye vyombo vya habari vya Kenya lakini sijui maana yake.

Naomba kuelimishwa.
 
Weka Picha ya ugatuzi Mkuu tumuone yukoje kwanza.
 
Hili neno 'ugatuzi' huwa nalisikia sana kwenye vyombo vya habari vya Kenya lakini sijui maana yake.

Naomba kuelimishwa.

ugatuzi maana yake ni baloz wa nyumba kumi ndugu
 
Ugatuzi ni devolution ,it is an administrative term!Al maarufu D by D,decentralization by devolution!

Watu wengine bhana...Ni sawa na Mtu anakuuliza Upepo ni nini? unamwambia Upepo ni maana yake Wind...

Wewe umeulizwa maana ya Ugatuzi na haujalizwa tafsiri ya neno Ugatuzi kwa Kiingereza! Sasa ukiulizwa na devolution maana yake nini utasemaje? Kwani umeambiwa kwamba sisi tunajua zaidi Kiingereza kuliko Kiswahili?
 

Ni kupeleka madaraka ktk ngazi ya chini mfano wilayani, halmashauri,kata, mitaa, vitongoji na kijiji
 
hoja alete mwingine afu ainoee uchungu mwingine?hii ni forum,mambo yanajadiliwa kwa namna mbalimbali na mwisho lengo linafikiwa,wewe usipolalamika siku yako haishi?hata kama nililoleta halikufaa mbele ya macho yako hiyo haikupi haki ya kuishusha hadhi hoja yangu!use your head and let your head to use you!usiwe mrahisi do not be cheap bhana,zingatia hoja na sio mleta hoja!ukiwa na lawama kuna sehemu za malalamiko uwe unapeleka lawama zako huko mkuu,with all the due respect ninaomba unisamehe kwa kukwaza mkuu!
 
Maana ya Ugatuzi ni kupeleka, kuhamisha, kuteremsha madaraka, mamlaka, kwa maana ya fedha, rasilmali watu, nyenzo, technologia n.k. kutoka Serikali Kuu (Central Government) na kuzipeleka chini kwa wananchi (grassroot)(Local Government/County Government) mfano kwenye vitongoji, vijiji na wilaya ili kuleta na kuharakisha maendeleo kwa nchi husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…