Nini maana ya upungufu wa nguvu za kiume?

namanyele

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
1,852
Reaction score
610
Habari wadau wa Jf,

Nina kijiswali ambacho mara nyingi huwa naulizwa na watu mtaani kuhusu upungufu wa nguvu za kiume, nilijua ni swali jepesi lakini pindi ninapojibu huwa napata changamoto nyingi sana.

Leo naomba mnisaidie kujibu hili swali. Ndani ya hili swali kuna viji maswali hapo chini vilijitokeza na ndiyo vilinipa wakati mgumu wa kutoa jibu sahihi.

1. Mwanaume anapochelewa sana au kuwahi kufika kileleni huyo ana upungufu wa kitu gani?

2. Akimaliza mzunguko wa kwanza inamchukua muda mrefu kusimamisha kwa ajili ya mzunguko wa pili au ndiyo mpaka
kesho tena, huyu naya ana upungufu wa nini ?

3. Wengine mbegu zao hazina uwezo wa kusababisha mimba, huyu naye ana upungufu wa nini?

4. Wengine wanatoa shahawa kidogo sana hata mzunguko wa pili akikojoa anaishia kutoa hewa tu, hawa nao wana upungufu wa kitu gani ?Nini maana halisi ya upungufu wa nguvu za kiume? tiba zake zikoje au tiba ya kitu kimoja inaweza kutibu vyote kwa wakati mmoja ?
 
Nguvu za kiume Kwa lugha nyepesi: Uwezo wa kufanya tendo ya ndoa kwa utoshelevu. Na inategemewa anapofikia mshindo atatoa mbegu. (bila kujali quality ya mbegu) nadhani hapo tofauti ya nguvu na mbegu iko wazi

Sasa Mwanaume akishindwa kufanya kwa utoshelevu ndio yaweza semwa kama upungufu japo yawezekana sio upungufu kama upungufu bali kutokufanya kwa uoshelelevu kumechangiwa na matatizo ya kisaikolojia kama stress, mazingiza, mdada, lishe (ameshiba sana) nakadhalika au baadhi ya magonjwa ya muda mfupi.

Ikiwa atashindwa kufanya kwa utoshelevu (subjective term) kila wakati, huyu waweza sema ana upungufu wa nguvu za kiume ambao pia unatibika kulingana na source yake.
 
Samahani nina swali, hivi kama mwanaume itasemekana anaupungufu wa nguvu za kiume, je mda huo huo kashindwa kuendelea na tendo ndani ya dk 3 za kwanza ukimpa chuma pia anakua hawezi kubeba? au hizo nguvu ni tofauti na za kubeba chuma. samahani kwa swali la kitoto
 
Karibu.

Anaweza beba chuma mgongoni huku anaendelea na zoezi hahaha
Libido ni tofauti na nishati ya kawaida inayoendesha mwili wa mwanaume. Kuwa na upungufu wa nguvu za kiume haumaanishi mwili hauna nguvu za kujiendesha kama kaiwaida, Hapana bali viuongo vya uzazi vya mwanaume ndio vinakuwa havina uimara tena wa kuendelea kwa wakati huo. Kuna tofauti kubwa kati ya nguvu mwanaume anayotumia say kukubeba, 'pumping' :yo:... ambazo zinategemea nishati ya mwili na uimara wa misuli na uwezo wa viungo vya uzazi kuwa imara kadiri matumizi yake yanavyotakikana. wataalamu wa afya wataeleza kwa uzuri zaidi hapo.. Am just a lay man.

Una umri gani Tamalisa?
 
upungufu wa nguvu za kiume ni kushidwa kusimamisha vzr, ukosefu ni kushindwa kusimamisha kabisa.
 
Karibu.

Anaweza beba chuma mgongoni huku anaendelea na zoezi hahaha
Libido ni tofauti na nishati ya kawaida inayoendesha mwili wa mwanaume. Kuwa na upungufu wa nguvu za kiume haumaanishi mwili hauna nguvu za kujiendesha kama kaiwaida, Hapana bali viuongo vya uzazi vya mwanaume ndio vinakuwa havina uimara tena wa kuendelea kwa wakati huo. Kuna tofauti kubwa kati ya nguvu mwanaume anayotumia say kukubeba, 'pumping' :yo:... ambazo zinategemea nishati ya mwili na uimara wa misuli na uwezo wa viungo vya uzazi kuwa imara kadiri matumizi yake yanavyotakikana. wataalamu wa afya wataeleza kwa uzuri zaidi hapo.. Am just a lay man.

Asante mkuu sasa nimeelewa
 
Mimi nafikiri neno "upungufu wa nguvu za kiume" ni neno ambalo limekuwa likitumika kwenye jamii yetu kuelezea hali tofauti tofauti ambazo mwanamme anaweza kuwa nazo ambapo hawezi kufanya tendo la ndoa cha kutosheleza. Ni kama mwavuli ambao umefunika vitu vingi chini yake. Nafikiri mwanamme akiwa na tatizo lo lote kati ya haya chini, ataambiwa hana nguvu za kiume:

1. Uume kushindwa kusimama kabisa, kusimama ukiwa hauna nguvu au kusimama kwa muda mfupi tu (Erectile dysfunction).

2. Mwanamme kufika kileleni mapema sana au hata kabla ya kuanza tendo (Premature Ejaculation)
3. Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa (Loss of libido)

Pengine unaweza kujumuisha hapa wale wenye tatizo la kuwa la upungufu wa mbegu (Low sperm Count) au wenye mbegu ambazo si komavu

Kila moja katika hayo ya juu ni tatizo tofauti kabisa na jingine na tiba yake ni tofauti kabisa. Vyanzo vya matatizo vyaweza kuwa ni vya kisaikolojia, matatizo katika mfumo wa homoni, maambukizi ya vijidudu au katika ufanyaji kazi wa mwili kwa ujumla.

Huwa nayajadili haya kwa kina katika tovuti yangu. Ukipenda unaweza kuitembelea http://www.sagalawebs.com/afya
 
Ukitaka kujua maana yake n nn,, nenda kajaribu kumdinya mke wa mganga ndo utapata tafsiri halisi
 
Back
Top Bottom