J JamiiTalks JF Advocacy Team Joined Aug 7, 2018 Posts 685 Reaction score 1,124 Mar 2, 2021 #1 USAWA: Ni hali ya kuwapatia wananchi wote fursa sawa katika kushiriki kwenye mambo yanayohusu jamii yao. Usawa katika utendaji unahusisha mambo yafuatayo: • Kutoa huduma bila ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote. • Kuendesha shughuli za umma bila ubaguzi au upendeleo. • Kuthamini watu wote bila kujali tofauti zao. • Kutambua makundi yote katika jamii na kutoa fursa sawa kwa makundi yote katika kuboresha hali zao. • Kumfanya kila mwanajamii kujiona kuwa yeye ni sehemu ya jamii na pia ana maslahi kwenye jamii yake. Upvote 0
USAWA: Ni hali ya kuwapatia wananchi wote fursa sawa katika kushiriki kwenye mambo yanayohusu jamii yao. Usawa katika utendaji unahusisha mambo yafuatayo: • Kutoa huduma bila ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote. • Kuendesha shughuli za umma bila ubaguzi au upendeleo. • Kuthamini watu wote bila kujali tofauti zao. • Kutambua makundi yote katika jamii na kutoa fursa sawa kwa makundi yote katika kuboresha hali zao. • Kumfanya kila mwanajamii kujiona kuwa yeye ni sehemu ya jamii na pia ana maslahi kwenye jamii yake.