Nini maana ya Ushirikina kwa mujibu wa vitabu vitakatifu?

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Ahlan wa sahla

Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu Torati, Zaburi, injili na Quran , Mungu amekemea sana kuhusu hii dhambi ya ushirikina.

Ama kwa hakika ndio amri ya kwanza aliyopewa Musa ktk zile amri kumi ili awaongoze wana wa izraeli.

Kwenye kitabu kitakatifu cha Quran vivyo hivyo imekemewa sana dhambi ya USHIRIKINA ,na Mungu amesema kuwa anasamehe dhambi zote kwa waja wake ila sio dhambi ya yule anayekufa ilihali hajatubia USHIRIKINA wake na pia amesema kuwa ameifanya PEPO (Paradise) kuwa ni haram kwa mshirikina.

Yaani ni bora ya mzinzi ,mwizi,kahaba au muuaji kuliko yule ambae ni mshirikina.Na mwisho akasema kuwa ushirikina ni dhulma kubwa sana.

Sasa kwa pamoja naomba ufafanuzi kutoka kwenu ,nini maana ya ushirikina kwa mujibu wa naandiko matakatifu.

Tanbih:
Naomba tujadiliane kwa amani pasi na kutukanana au kukejeli maandiko matakatifu.

Katibuni: uzi tayari
 
Kwa mujibu wa uislam,ushirikina(shirk) ni kitendo chochote Cha kumpa asiyekuwa muumba(Allah) haki anazopaswa kupewa yeye pekee(kuabudiwa).
Ni dhambi kubwa kuliko zote ambayo ikiwa mtu hatubii Basi hatosamehewa

ۖإِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru. [Al-Maaidah: 72]
 
Back
Top Bottom