1. Ni wale tuliye nyanyaswa wa wakoloni zamani za wazazi wetu na hatukua na nguvu ya kumpiga mkolonibau kumfukuza kw lazima kwa kukosa elimu,pesa na uwingo wa wananchi,jambo hilo ni sehemu ya neno Mnyonge
2. Wengi ni wenye kipato cha chini wasio na sauti mahala popote kwa kua katika hali ya kawaida mtu asiye na pesa hua hana sauti kwenye jamii na wala mapendekezo yake hata kama yana tija hudharauliwa na kufanya watu wenye pesa na vyeo maofisini wachukue nafasi za kila kitu kua ndio wasemaje na hata wanaweza kupora mali ya hawa wasio na sauti kwa sababu ya kukosa kwao fedha na elimu,huu ni Unyonge.
3. Walemavu wa viungo,akili na kadharika ni sehemu ya Unyonge
4. Ukiwa mnyonge kwa maana chache nilizozitaja hapo juu wenye nguvu ya fedha na vyeo wanaweza wakachukua na cha kwako wakaishia nacho,wanawwza wakabeba mke/mume wako,wanaweza wakabeba aridhi yako na hata uhai wako iwapo utawagusa katika maslahi yao.
5. Rais tulienaye ni mtu anaye jitahidi kuweka usawa na kutupa msukumo wa kila mmoja kufanya kazi kwa bidii na usawa katika nafasi yake,anaweka na heshima kwa kila mmoja kumheshimu mwingine.ndiyo maana MUNGU mwenyewe aliwahi kusisitiza upendo,kitu amabacho watu wote kama wananchi tukikibeba kitatufanya kuishi kwa usawa bila kupokonyana mali wala kunyanyasana katika maeneo ya kazi na majumbani mwetu
"SIKU NJEMA"