Nini madhara ya kunywa maji lita 6 kwa siku?

Asante mkuu
 
Mbona siwaelei, mimi ni 88kg na sina kisukari wala presha ila nakunywa maji 4.5l per day yaani chupa 3 za maji ya kilimanjaro makubwa. Nishazoea na imekua sehemu yangu ya maisha kunywa maji mengi maana sinywi kinywaji chochote zaidi ya maji.

Kusema kunywa maji mengi ni kisukari siwaelei na sifanyi kazi ngumu.
 
Ampeleke hospitali au amshauri kwenda hospitali? mwanaume/mwanamke wa miaka 45 ambaye hayuko hoi kwa ugonjwa anapelekwa hospitali?
Amesema mdogo wake itabidi ampeleke hospitali kupima atamshauri atakubali ushauri wake? wakati yeye anajiona mzima kwa kunywa maji mengi namna hiyo? Mkuu Tujalie wewe ndio mdogo wako utaweza kumshauri aende hospitali? je akikwambia haumwi na kitu?
 
Bado naamini anatakiwa kumwelewesha kuwa kuna tatizo ili akubali kwenda hospitali kuangalia afya yake...after all, amesema alishakwenda hospitali ya Mulago Uganda. Vinginevyo mkuu, unafikiri atawezaje kumpeleka mdogo wake wa miaka 45 hospitali 'kwa lazima'? Ndiyo maana nafikiri itabidi amshauri, baada ya kumwelewesha madhara ya hali hiyo. Huyo ni mtu mzima saana si mtoto wa kuambia "twende hospitali mara moja!"
 
Kunywa maji angalau lita tatu kwa siku hasa kwa wenye uzito wa kawaida unaoendana na urefu wao, ukinywa maji mengi kupitiliza unazifanya figo ziwe overworked na hivyo unaweza kuleta madhara kwa figo hapo baadae. Kunywa maji mengi hakuhusiani moja kwa moja na ugonjwa wa kisukari...
 
Mkuu hata huyu dogo wangu hana ugonjwa wa aina yoyote ile,ana kilo 106,anakunywa lita 6 kwa siku yaani chupa 4 za Kilimanjaro.
 
Ina maana hawa wanaojitangaza kwenye tv kuwa ni wataalam wa tiba mbadala wanatupotosha?
 
Unatakiwa Kunywa Maji kulingana Na Uzito wako si Kubugia Maji Tu.. Utakuwa Unakojoa Na Madini ya Mwili Sasa

Mfano Mwenye Uzito wa 60kg Anatakiwa Kunywa Maji lita 2.5 asizidi hapo..

Unakokotoaje sasa!?
 
Mkuu kuna ile kanuni ambayo inasema uzito wako unatakiwa uendane na urefu wako, kama unaifahamu pliz naomba unisaidie kuniambia. Natanguliza shukran zangu za dhati
 
Navyojua kisukari...huambatana na kiu kali...hio ndio inampelekea mtu kunywa maji mengi...lakini kuna wale wanakunywa just sio kwa kiu...ila..kwa sababu ya kiafya tu(WATER THERAPY)..! binafsi hua nakunywa...lita 3 ad 5(1 gallon) kwa siku..sio kwakua nina hisi kiu...hapana...lakini kiafya..maji ni muhimu..ukizngatia mwili wa mwadamu ni maji asilimia kubwa! BUT maji tunywe kwa viwango...maaana pia kuna Madhara kama water intoxication
 
Madhara ya kunywa maji mengi yasiyo endana na uzito wako ni maji kujaa kwenye mapafu na kupungua kwa baadhi ya madini mwilini kwa kuwa atakuwa anakojaoa mara kwa mara.
 
Mkuu kuna ile kanuni ambayo inasema uzito wako unatakiwa uendane na urefu wako, kama unaifahamu pliz naomba unisaidie kuniambia. Natanguliza shukran zangu za dhati
Body mass Index(BMI) google hilo neno utapata formula hapo
 
Mkuu kuna ile kanuni ambayo inasema uzito wako unatakiwa uendane na urefu wako, kama unaifahamu pliz naomba unisaidie kuniambia. Natanguliza shukran zangu za dhati

BMI, Body Mass Index! Itafute hiyo then jaza mass yako na urefu wako utajua kila kitu...
 
Thanks sana mkuu.
Naweka chumvi ya aina gani kubalance ions za mwili?
Si unajua hizi chumvi za unga from China zadaiwa kupunguza nguvu za kiumeni?
 
Drinking excessive water is not good for your health as this weakens the ability of the kidneys to excrete excess water load and sodium in the body becomes diluted. This leads to swelling in cells, which can be life-threatening.
 
BMI, Body Mass Index! Itafute hiyo then jaza mass yako na urefu wako utajua kila kitu...

BMI is calculated as weight/height squared...bmi values are underweight=<18 normal=18.5-26 overweight 26.5-30 obesity type 1=30.5-34.5 obesity type2=>35 we use these values across all kenyan hospitals..thanx
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…