Heh Kichankuli,
Kila siku nasoma yahoo news na ninaona maraisi wa nchi kama USA, USA,GERMAN, JAPAN wanapotoa matamko kuhusu hatua wanazochukua kunusuru nchi zao na Recesion. Nasikia mara wamepunguza makato ya kodi kwa viwanda vya ndani au kilimo, pia wamekata/wamepunguza matumizi ya serikali. Pia wamepunguza mishahara na posho za viongozi.
Sasa hapa Tanzania tu nasikia mambo ya mapapa, nyangumi. Sioni la maana. KWanza namuunga mkono Cheyo kwa kusema hao watuhumiwa wakamatwe kwanza, pia wavuliwe uanachama kwanza halafu ikiwa watathibitika kuwa si wahalifu, ndipo waombe uanachama upya. Mahakama pekee ndio inaweza kuwasafisha.
Hapa Tanzania sioni mikakati ya kiuchumi, ni siasa tu.
Nakumbuka wakati marekani inaanza kupatwa na misukosuko ya kiuchumi, Mh MKulo na Prof Ndulu walisema msukosuko hautaikumba Tanzania. Wanaongea tu basi ili mradi siku imepita na swali halipo.
So natoa wito kwa viongozi kuacha siasa kwenye issue muhimu za uchumi.