Nini matokeo ya Waziri Mkuu Majaliwa kukutana na Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma?

Nini matokeo ya Waziri Mkuu Majaliwa kukutana na Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma?

KASULI

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
599
Reaction score
677
Mapema Januari mwaka huu Waziri Mkuu alitoa ufafanuzii juu ya kile kinachoitwa bodi ya mishahara ilii kurekebisha mishahara iendane na elimu na ugumu wa kazi.

Leo ni Desemba hakuna tamko au chochote kipya.

========

Alhamisi, Januari 24, 2019

Majaliwa akutana na wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.

Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.

Amekutana na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi, Januari 24, 2019) katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi kwa bidii.

Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa umma nchini.

Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye utumishi wa umma.

“Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.”

Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi mazuri.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

TUJIULIZE: Nini kiliipata Bodi hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kama vile ilivyokuwa uhakiki wa watumishi hewa ni 'delay tactics' za serikali ya Magufuli za kukwepa kuongeza mishahara ya watumishi. Nothing new.
 
Kama kwenye hicho kikao chao hao wajumbe wa bodi walikunywa chai au kula limao na pia wakaahidiwa chai au limao nyingine usitegemee lolote la maana kutoka bodi hiyo. Tafakari.
 
Kama kwenye hicho kikao chao hao wajumbe wa bodi walikunywa chai au kula limao na pia wakaahidiwa chai au limao nyingine usitegemee lolote la maana kutoka bodi hiyo. Tafakari.
Hii kituu
 
Back
Top Bottom