karv
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 1,802
- 3,253
Habari wana JF leo naomba nizungumze kitu ambacho binafsi kinanikera sana na huwa sikielewagi
Kitu chenyewe ni kuhusu muitikio wa serikali katika kuzisapoti timu zetu za taifa hasa mpira wa miguu
Kwanza naomba kurudi nyuma kidogo wakati wa utawala wa rais Kikwete aliajiri makocha wa timu za taifa kwa kila mchezo hadi mpira wa pete(netball kama sijakosea)
Nakumbuka kipindi hicho Tanzania tulipanda viwango vya FIF hadi nafasi ya 91 duniani licha ya kwamba hatukuwahi kufuzu AFCON nakumbuka tulifungwa na Msumbiji uwanja wa Taifa kwa sasa uwanja wa Benjamin Mkapa kipindi hicho bado mpya ila serikali ilitoa sapoti sana kwa wakati huo
Katika utawala wa hayati Magufuli & Samia mambo yakawa tofauti kabisaaa licha ya timu zetu za Taifa kufuzu AFCON lakini bado mchango wa serikali ni mdogo sana katika sekta ya michezo sio tu mpira wa miguu hata michezo mingine
*Nani asiyejua kama tulikosa watu wa kutushikia hata bendera kule Olimpic
*Nani asiyejua Biashara United Mara wametolewa Kombe la shirikisho kwa kukosa nauli tu ya kwenda libya
*Nani asiyejua kama Mkwasa na Emannuel Amunike walikuwa wanacheleweshewa mishahara na TFF(Rejea hotuba ya waziri wa zamani wa michezo Mh Dkt Mwakyembe ya Baada ya timu kurudi kutoka AFCON)
*Nani asiyejua kama vifaa vya michezo havijaondolewa kodi
*Nani asiyejua mechi ya Simba na Yanga ilisogezwa mbele muda kisa tu Mh Mwinyi anazindua kitabu chake
*Nani asiyejua kama TFF ndio wanawalipa makocha wa timu za Taifa mishahara
*Nani asiyejua kama gharama za kambi na posho za wachezaji wa timu za taifa ni jukumu la vyama husika vya mchezo huo
*Nani asiyejua kwamba timu za taifa zikifungwa lawama zinatupwa kwa vyama husika vya mchezo huo na wala sio serikali iliyoshindwa kutoa sapoti
*Nani asiyejua kwamba michezo Tanzania imetawaliwa na siasa nyingi
Sasa kazi ya serikali na wizara ya michezo ni ipi
*Kuzipa bendera timu za Taifa zinaposafiri?
*Kuzialika timu ikulu na kuwanunulia viwanja baada ya kushinda makombe ambayo hawajui hata yamepatikana vipi?
*Kuanza kutafuta ujiko na kuunda kamati pindi timu zetu tunapoanza kuonyesha mwanga wa mafanikio?
*Kuzuia nyasi bandia kwa sababu hazijalipa kodi?
*Kushindwa kupunguza kodi kwa vifaa vya michezo?
*Kuleta ahadi hewa na siasa katika kukuza michezo nchini?
*Kusimamia chaguzi za viongozi wa soka?
*Kuita timu bungeni baada ya kufanya vizuri?
*Kuunda kamati na slogan mbali mbali?
Tatizo la serikali yetu na wadau wa michezo ndio hilo timu inapoanza mashindano ni ya TFF ikifikia hatua ya matumaini ndio watu fulani fulani wanaaza kujitokeza
Mfano
*Mh waziri mkuu ulikuwa wapi tangu Taifa stars inaenda kucheza DRC congo, ikacheza na madagascar ikacheza na Benin ila baada ya kuona inaenda kwenye mafanikio ndio mnajikuta serikali mnajali saaana michezo
*Mh Rais Samia wakati Twiga stars inaenda kucheza COSAFA ulikuwa wapi hadi wanarudi na kombe ndio unaanza kujipendekeza na kuwapa viwanja huo ni unafiki mkubwa je wasingeshinda hivyo viwanja wasingepewa
*Samia wakati ukiwa makamu wa rais hukuwaona vijana wa Serengeti boys hadi walipofuzu kwenda Gabon ndio ukawaita waje kula ikulu
Michezo ni ajira hivyo ili sekta ya michezo nchini iweze kukua yanahitajika maandalizi ya muda mrefu ikiwezekana hata miaka 10 na serikali ingefanya yafuatayo
*Kuondoa/kupunguza kodi kwa vifaa vya michezo na nyasi bandia nchi nzima sio tu kwa majiji kama ilivyo sasa
*Kulipa mishahara kwa makocha wa timu za taifa vyama vya michezo wao wawe na kazi ya kutafuta hao makocha mfn wakati wa rais Kikwete
*Sapoti na hamasa zisiwe katika mafanikio pekee bali yaanze tangu mwanzo na yawe endelevu
PONGEZI
Pamoja na mapungufu yoyote haya kuhusu suala la timu za taifa hasa Taifa stars naomba kuwapongeza wafuatao
*Mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa utawala wake alijali sana michezo
*Nape Nauye enzi akiwa waziri wa michezo alijitoa sana kwa Serengeti boys hadi kufikia pale ilipofika
*Dkt Mwakyembe naye alijitoa sana na alikuwa mfuatiliaji katika timu ya Taifa stars
*Paul Makonda huyu mchango wake katika kukuza soka chini ni mkubwa sana rejea eneo la Yanga kigamboni na Lile alilowapa TFF
*Hayati Mzee Mkapa kwa kujenga uwanja wa Taifa mkubwa na mzuri
NB: ILA HAPA KWA Bashungwa tumepigwa na kitu kizito ni mzuri kwenye kuongea ila vitendo ni sifuri haigi hata kwa watangulizi wake analeta siasa hadi kwenye michezo
Niitakie heri timu yetu ya Taifa stars kuelekea mchezo wao dhidi ya DRC CONGO
Kama kuna sehemu nimekosea ni maswala ya uandishi tu na kumbu kumbu
NAOMBA KUWASILISHA