Nini nifanye

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
1,889
Reaction score
3,059
Kuna uzi nilileta juu ya maisha yangu kuwa magumu na bila msaada

Sasa kuna kazi nilisema ninafanya sikuiacha niliendelea nayo na nimelipwa pesa yangu ila sina mpango wa kuiacha nataka niendelee nayo huku nafanya Biashara nyinginee

Wakuu hapa nina laki 2 kamili nataka niizungushe kwenye Biashara ya nguo angalau nisikose kabisa pesa ya kula

Nimewaza nifanye Biashara ya mtumba nguo za kike au nguo za watoto wadogo wa kiume

Nguo za kike nazotaka ni zile za fashion za wadada wachuo vigauni vya kichuochuo yaani wateja wangu wawe wanafunzi wa vyuoni ila niifanye kwa njia ya online

Naombeni ushaurii na namna ya kupata soko la kununua hizo nguo kwa bei nzuri

Au Kama kuna mwenye ushaurii wa Biashara nzuri kwa mtaji huo wa laki 2
 
Kwa wanachuo sasa hivi umechelewa ndgu, vyuo vinafungwa sio mda mrefu na Gen Z wanarudi makwao.

Hiyo target yako ya wanachuo ifanye kuanzia Nov.

Nikiuzia online siwezi kupata wavaaji hata wadada ma slay queen [emoji16]
 
Your gender?
 
Una hiyo platform ya kuuza online kama page au account yenye wateja wa namna hiyo??

Mzee tatizo lako unataka kesho tu uanze kula midusko uwe tajiri.
Hizi mambo zinaanza chini kabisa.

Tengeneza jina kwanza.

Sasa si ndio naanza mdogo mdogo wewe sasa unasema nisubiri mpk mwezi November inamaana nisifanye Biashara nikae tu na hiyo hela

Ndio hizo platform mnielekeze

Hapa nilipanga niwe nalipia matangazo fb napost kwenye groups
 
Sasa si ndio naanza mdogo mdogo wewe sasa unasema nisubiri mpk mwezi November inamaana nisifanye Biashara nikae tu na hiyo hela

Ndio hizo platform mnielekeze

Hapa nilipanga niwe nalipia matangazo fb napost kwenye groups
Kama target yako ni wanachuo ukweli ndo huo ndgu yangu labda ubadili aina ya wateja unaotarget.

Yaani ni sawa na uende kufungua biashara yako nje ya geti la IFM pale posta ukitegemea wanachuo wakuungishe, utapata hamna maana sio mda wanafunga na vyuo mara nyingi hubaki vitupu.

Fungua account fb au insta, anza kua kama mawinga, unapost bidhaa yako(ambayo ipo dukani kwa mtu) mteja akiipenda analipia/ unampelekea analipia.
Unatengeneza faida wakati huohuo unatafuta wateja wako wanaokuamini.
 
Hiyo biashara ya nguo ni risk sana ukizingatia na mtaji wako..
..chukua laki na nusu tafuta odds kumi utakuja kunishukuru baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…