Nini sababu ya 90% ya wakopaji kushindwa kurejesha mikopo yao?

Nini sababu ya 90% ya wakopaji kushindwa kurejesha mikopo yao?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Kuna jambo la kustaajabisha sana kuhusiana ya mikopo, mara nyingi mikopo hailipwi kwa sababu zisizoeleweka na imepelekea baadhi ya watu kuona kuwa mikopo ni matatizo katika maisha yao huku wengine wakidai fedha za mikopo hazina baraka nakadhalika.
Je, wewe una lipi la kuzungumzia juu ya swala hili?
 
kuna mwamba alikopa alafu akaenda kununua gari marejesho anategemea mauzo ya duka lake ndo apeleke,mwisho wa siku aliuza tena gari amalizie mkopo.
 
Wakati wa kukopa inabidi uangalie na sehemu unayokopa, Kuna sehemu nyingine ukikopa basi hutolipa kamwe mpaka ulichoweka bond kinachukuliwa
 
Kuna jambo la kustaajabisha sana kuhusiana ya mikopo, mara nyingi mikopo hailipwi kwa sababu zisizoeleweka na imepelekea baadhi ya watu kuona kuwa mikopo ni matatizo katika maisha yao huku wengine wakidai fedha za mikopo hazina baraka nakadhalika.
Je, wewe una lipi la kuzungumzia juu ya swala hili?
Kwa maoni yangu kuna sababu kama mbili tatu hivi, mfano:

1. Kutokujipanga mapema, yaani mtu anahemkwa kwenda kukopa wakati hata hajapanga vyema matumizi ya huo mkopo wenyewe, matokeo yake anashindwa kuurejesha;

2. Kuutumia mkopo kwa manunuzi ya vitu vyengine, umekopa kwa ajili ya kuendeleza biashara lakini unaishia kwenda kununua viatu na television.

3. Kukopa kwa ajili ya ununuzi wa vitu ambavyo havileti faida, mfano ujenzi wa nyumba, ununuzi wa gari.

4. Riba kubwa kuliko hicho kinachopatikana wakati wa kurejesha mkopo. Kuna baadhi ya taasisi zinakopesha kwa riba mpaka asilimia 40, wengine ati asilimia 10 kwa wiki - hebu piga hesabu uone hizo fedha utakazokopa na utakazorejesha ni ngapi? Utashangaa umerejesha karibu mara mbili ya ulizokopa.
 
Back
Top Bottom