demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Ni kuhusu Ibrahim Ajibu.....wengi humwita [SonOfGod]...
Huyu dogo amekuwa akifanya vyema sana tangu alipojiunga na Mabingwa watetezi, Mabingwa wa kihistoria wa mpira wa miguu Tanzania Bara.
Amekuwa akionyesha kiwango ambacho walio wengi (mashabiki kutoka pande zote) wanathubutu kukiri kuwa hakuwahi kabisa kukionyesha kipindi anawatumikia mabingwa wa mwaka 2012.
Nilipata nafasi ya kuongea na mtu wa karibu wa familia yake ambaye alithibitisha kuwa Ajibu hawahi kuwa na furaha katika kipindi chote alicho kuwa akiwatumikia Mabingwa hao wa mwaka 2012. Sababu kubwa ni klabu yake hiyo kushindwa kumthamini kwa namna ambavyo klabu ya Yanga inamthamini hivi sasa, akitanabaisha zaidi ndugu huyo anasema "Ki uhalisia hiyo ndio sababu kuu ya kuwa na viwango tofauti, pia ushabiki na upenzi huenda ikawa kichochezi cha ziada kwake kufanya vyema akiwa Yanga, Unajua Ajibu amekuwa ni shabiki na mpenzi wa Yanga tangu akiwa kijana."
Ibrahimu ajibu amejiunga na Yanga msimu wa 2017/18 kuchukua nafasi ya Kiungo Niyonzima aliye elekea upande wa pili katika usajili ulioshika vichwa vya habari ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Usajili huo ulifanywa kwa makusudi kabisa na viongozi wa Yanga ili kutekeleza sera mpya ya Mabingwa hao watetezi na wa kihistoria ya kuwa na viungo wenye uwezo wa kufunga wastani wa magoli 9 hadi 16 kwa msimu mmoja....na kuondoa viungo wasio endana na sera hiyo mpya ya Klabu.
Ibrahim Ajibu anaonekana kufanya vyema zaidi kuliko mchezaji aliyeelekea upande wa pili....
NB; Kwa upande wako, kwa namna uonavyo. Nini sababu ya Maestro huyu wa kitanzania kufanya vyema akiwa Jangwani kuliko alivyokuwa Matopeni FC?