Nini sababu ya Ajibu kufanya vyema akiwa Jangwani.?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Ni kuhusu Ibrahim Ajibu.....wengi humwita [SonOfGod]...

Huyu dogo amekuwa akifanya vyema sana tangu alipojiunga na Mabingwa watetezi, Mabingwa wa kihistoria wa mpira wa miguu Tanzania Bara.

Amekuwa akionyesha kiwango ambacho walio wengi (mashabiki kutoka pande zote) wanathubutu kukiri kuwa hakuwahi kabisa kukionyesha kipindi anawatumikia mabingwa wa mwaka 2012.

Nilipata nafasi ya kuongea na mtu wa karibu wa familia yake ambaye alithibitisha kuwa Ajibu hawahi kuwa na furaha katika kipindi chote alicho kuwa akiwatumikia Mabingwa hao wa mwaka 2012. Sababu kubwa ni klabu yake hiyo kushindwa kumthamini kwa namna ambavyo klabu ya Yanga inamthamini hivi sasa, akitanabaisha zaidi ndugu huyo anasema "Ki uhalisia hiyo ndio sababu kuu ya kuwa na viwango tofauti, pia ushabiki na upenzi huenda ikawa kichochezi cha ziada kwake kufanya vyema akiwa Yanga, Unajua Ajibu amekuwa ni shabiki na mpenzi wa Yanga tangu akiwa kijana."

Ibrahimu ajibu amejiunga na Yanga msimu wa 2017/18 kuchukua nafasi ya Kiungo Niyonzima aliye elekea upande wa pili katika usajili ulioshika vichwa vya habari ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Usajili huo ulifanywa kwa makusudi kabisa na viongozi wa Yanga ili kutekeleza sera mpya ya Mabingwa hao watetezi na wa kihistoria ya kuwa na viungo wenye uwezo wa kufunga wastani wa magoli 9 hadi 16 kwa msimu mmoja....na kuondoa viungo wasio endana na sera hiyo mpya ya Klabu.

Ibrahim Ajibu anaonekana kufanya vyema zaidi kuliko mchezaji aliyeelekea upande wa pili....





NB; Kwa upande wako, kwa namna uonavyo. Nini sababu ya Maestro huyu wa kitanzania kufanya vyema akiwa Jangwani kuliko alivyokuwa Matopeni FC?
 
Yanga anasajili kocha.
Matopeni anasajili Makofia akishauriana na Kaburu Voster!

Kocha ndiyo anajua mchezaji atafiti vipi kwenye mfumo au falsafa yake. Si ajabu Ajibu kufanya vizuri maana kocha alijua atamtumia vipi.
 
Yanga anasajili kocha.
Matopeni anasajili Makofia akishauriana na Kaburu Voster!

Kocha ndiyo anajua mchezaji atafiti vipi kwenye mfumo au falsafa yake. Si ajabu Ajibu kufanya vizuri maana kocha alijua atamtumia vipi.


Ndio maana siku hizi namuona Mkude kwenye mechi zao....

Zile kelele za Mashabiki zimewafikia viongozi, Viongozi wakapeleka jina kwa Omog kwamba huyu mtu ni lazima acheze.😀😀
 
Muulize mwenyewe Ajibu, siri anayo yeye, ila kimtazamo Ajibu hakuondoka vizuri Simba na alipofika kwa Vyura fc kulikuwa na minong'ono kwamba hataweza kucheza vizur kwani bado alikuwa anampenda mnyama - nguvu moja hivyo ili kujiridhishia nafasi na ubora ilimbidi aongeze bidii mara dufu.
Hapo ambao walishawahi kugusa mpira watanielewa, woga wake ndio juhudi zake mwishowe ndio tunamuona huyo Ajibu alivyo sasa.
Mambo ya kuendekeza ....nadhani amepunguza.

Ajibu ni mchezani mzuri, alilelewa na Mnyama, usimlishe imani isiyo yake.
Ipo siku utakuja kujuta, kumbuka siku ya Simba Day Ajibu alikuwaje ndio ujue huko yupo kikaz sio kishabiki.
Mfuatilie vizuri utajua.
Mwisho; usiwaamini sana wachezaji wazuri wa mpira.
 
mahabaa yake kwa team anayoipenda kabisaa kutoka moyoni kwake yaaniii Dar Young Africa........achaaa kabisaaa!
 
Ndio maana siku hizi namuona Mkude kwenye mechi zao....

Zile kelele za Mashabiki zimewafikia viongozi, Viongozi wakapeleka jina kwa Omog kwamba huyu mtu ni lazima acheze.😀😀
Bahati nzuri upuuzi huo haupo Yanga. Matunda yake ni ndoo tatu mfulilizo. Ya nne ipo njiani kuanzia Jumamosi hii
 
Ajib ni mchezaji mzuri toka alipokua Simba.

Utofauti unaouona ni kua simba ni team work hivyo ni nadra sana kumuona mtu mmoja akiwazidi sana Wenzie.

Nakubwa zaidi kwasasa nikua Yanga haiko sawa Sana hivyo inampasa yeye kufanya kazi za midfield na strikers freekicks corners na vingine,

Simba midfield inafanya kazi zake sawia hivyo yeye hakua nakazi kubwa yakusaidia eneo hilo.

Na mifumo ya simba yeyote anakufunga ndio maana wachezaji wengi waligawana magoli msimu uliopita.

hivyo vinamfanya ashiriki kwenye sehemu kubwa ya mchezo.

Nahapo ndipo macho yote sasa humwangalia yeye.
 
Umeongea vizur mkuu pata like yangu
 
Sasa nimehamia timu ya sasa......
Toka ile timu niliyokuwa zamani....
ile timu sio timu ilikuwa na mikosii eeeee......
zengwe zengwe haziishi kila siku tuchezapooo....
Njaa njaaa haziishi.. Kila siku eeeeee......

Saha nimehamia timu ya sasaaa.....
Mechi zote nacheza na kufunga.....
Mabosi wameniongeza na mafao....
Mashabiki nao wananituza.....
 
Hahaha nimecheka hio picha eti anamuiga messi ma ronaldo...

Kibongongo hutokosea kumuita Ronaldo. Jaribu kuufungua moyo wako, mpe anachosahili. Hata kama aliwahi kuchezea Simba.
 
Nakubwa zaidi kwasasa nikua Yanga haiko sawa Sana hivyo inampasa yeye kufanya kazi za midfield na strikers freekicks corners na vingine,



Viungo wa kisasa ulimwemguni ni lazima uwe na uwezo ambao ajibu anao, na sio vinginevyo. Kuingo wa kisasa ni lazima uwe unauwezi wa kuamua matokeo bila kutegemea uwepo wa washambulizi.

Kiungo wa kisasa naturally uwe na uwezo wa kupiga free kicks (ambapo by defaulty ukiwa mpigaji freekick mzuri basi hata kona unaweza piga)

Nafasi anayocheza Ajibu pale Jangwani ni sawa na anayocheza Okwi pale kwenu. Sasa niambie kuwa simba nayo haiko sawa hata inampasa Okwi kufanya kazi za akina Mavugo, maana yeye mfungaji kiongozi, hupiga freekick zote, na hata baadhi ya kona huzipiga yeye.

Ajibu, Msuva na Okwi ni mfano wa viungo wa kisasa ulimwenguni. Ukiona kiunga hawezi kupiga freekick wala kutegemewa kuamua matokeo ujue hamna kitu humo.
 
Simba Day Ajibu alikuwa anafanya mazoezi na timu yake Yanga
 
Weka pembeni ushabiki kisha jaribu kufuatilia soka vizuri,Angalia heading yako na nilichokiandika Mimi utanielewa kila la kheri kwenye mechi ya kesho.
 
Pia chakula bora malazi safi na maji ya kutosha vinamfanya afanye vizuri
 
Yanga anasajili kocha.
Matopeni anasajili Makofia akishauriana na Kaburu Voster!

Kocha ndiyo anajua mchezaji atafiti vipi kwenye mfumo au falsafa yake. Si ajabu Ajibu kufanya vizuri maana kocha alijua atamtumia vipi.

Mkuu Sibonike! Kaburu Vorster! Nimechekaaaa mpaka basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…