Nini sababu ya jichi la kushoto kucheza?

Nini sababu ya jichi la kushoto kucheza?

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
888
Reaction score
821
Leo siku 26 mboni ya juu ya jicho la mkono wa kushoto linacheza cheza sana.

Naomba tafsiri kwa wajuvi wa mambo haya.

Enzi na enzi.
 
Ugonjwa huo. Mboni haikuumbwa icheze cheze. Au unasemaje?
 
Nijicho la juu na haliumi! Wanasema nikiashilia sasa natafta akina mshana jr nawengine watupe tafsiri.
 
Nijicho la juu na haliumi! Wanasema nikiashilia sasa natafta akina mshana jr nawengine watupe tafsiri.
Naona umefulia sasa unatamani ubashiriwe bahati nasibu za mafanikio. Maana ya mtikisiko huo ni kwamba haipiti wiki bila wewe kutusua mkwanja mnono, wa maana, tena unaletewa moja kwa moja hadi mlangoni. Juma zima usitoke wala usile na kunywa chochote hadi upewe chako.
 
Ha ha ha ha ! Mwanangu umetisha, naomba iwe hivyo.
 
Hiyo ni dalili ya mvua au msiba mkuu,jiandae kisaikolojia

Ingawaje inaweza kua tofauti na hayo kwani kitendo fulani kinaweza kuwa na ishara zaidi ya moja
 
Msiba ni jicho la chini, mvua huwezi tabiri saivi maana zinanyesha kila siku
 
Jua kuna ugomvi mkubwa sana wa kimapenzi unakuja, mkeo anachepuka kama umeoa. Au demu wako kazama kwenye penzi la mtu mwengine. Vice versa kwa mwanamke.
 
Jicho likicheza utaona vitu vibaya
Mkono ukiwasha utapata hela
Tuzi ikiwasha ujue utapata ..........
 
Jua kuna ugomvi mkubwa sana wa kimapenzi unakuja, mkeo anachepuka kama umeoa. Au demu wako kazama kwenye penzi la mtu mwengine. Vice versa kwa mwanamke.
USHINDWE KWA JINA LA YESU WA NAZARETH

MUNGU UTUEPUSHIE NA TAFSIRI HII NYENYEFU
 
Back
Top Bottom