Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Siku za hivi karibuni kumekua na vifo vingi vinavyohusiana na saratani.
Mwaka jana tulizika ndugu yetu,mwanamke wa umri wa miaka 46 aliyekuwa anasumbuliwa na saratani,aliugu muda mrefu pamoja na maumivu makali.
Juzi kuna kijiji nilienda kuna mama mmoja namfahamu ni mama mtu mzima umri miaka 64 nimeona ana uvimbe sehemu za shingoni kuelekea mdomoni kumuuliza anasema amekwenda hosp. Vipimo vinaonyesha ana saratani kwa hiyo akarudishwa nyumbani hadi sasa yupo nyumbani anasubiri lolote litakalotokea.
Jirani yangu mama mtu mzima ana kansa ya ziwa mwaka wa kumi huu,anasema baada ya vipimo kuonyesha ana saratani alianza kutumia miti shamba na hajawahi kukatwa ziwa lakini hadi leo anatumia miti shamba akiwa anaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Rafiki yangu aishie dar es salam mke wake ni mgonjwa wa kitandani sasa,alipata uvimbe kwenda kuutoa kumbe ilikuwa saratani baada ya hapo imeanza kusambaa mwilini, kila wiki ni kwenda kuchoma mionzi na pesa zinaishia huko,watoto wake bado wadogo, yupo hoi kitandani huku akijua nini kinafuata., mumewe muda mwingi ni kulia.
miti shamba gani itakayotibu cancer na watu wakapona maana hata wazungu wameshindwa.
Saratani shkamoo