Nini sababu ya kutotoka maziwa ghafla kwa mama anaenyonyesha??

Nini sababu ya kutotoka maziwa ghafla kwa mama anaenyonyesha??

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
2,845
Reaction score
2,024
Hellow doctors
Nini husababisha kutokutoka kwa maziwa kwa mama anaenyonyesha ikiwa mwanzo maziwa yalikua yanatoka vzuri tu,na anakula ipasavyo..maana friend of mine now ni siku ya tatu analalamika maziwa hayatoki nakula anakula ipasavyo!tunaomba msaada wenu na kipi kifanyike ili maziwa yatoke?maana mtoto analia hadi anakauka kwa kukosa maziwa.
 
Hellow doctors
Nini husababisha kutokutoka kwa maziwa kwa mama anaenyonyesha ikiwa mwanzo maziwa yalikua yanatoka vzuri tu,na anakula ipasavyo..maana friend of mine now ni siku ya tatu analalamika maziwa hayatoki nakula anakula ipasavyo!tunaomba msaada wenu na kipi kifanyike ili maziwa yatoke?maana mtoto analia hadi anakauka kwa kukosa maziwa.
Nlikua na hiyo kitu pia, nakunywa uji, nakunywa supu, mtori nashangaa hola hakuna kitu...
Nlikua nauchapa usingizi saa nne ndio nakula, hapo hata ule vipi maziwa hayatoki.

Kumbe kunyonyesha sio kula sana ila kula kwa wakati, inatakiwa kula mapema yani kumi,kumi na moja, kumi na mbili alfajiri mama anatakiwa awe amekula, pia asikae akasikia njaa akifanya hivo maziwa hayakauki.
 
The more unanyonyesha ndo maziwa yanazidi kutoka hypothalamus hapo.

Kuna maradhi pia yanashambulia maziwa ya mama na kuzuia maziwa kutoka,Mastitis,breast abscess/majipu haya,galactocele,breast cyst na pia homa kali.

Vidonge vya uzazi wa mpango hasa vile viko na Oestrogen hii hormone ipo na tabia ya kukausha maziwa not only pills but also njia nyingine za uzaz zenye oestrogen hormone.

Mawazo yaliyopitiliza/stress/anxiety nayo huchangia.

Kufanya kazi ngumu hasa za kutoka jasho huchangia mama kukosa maziwa.

Kutokula a well balanced diet.

Mshauri aende hospitali ili kama ni tatizo ni kubwa Mtoto apewe njia nyingine za ulaji.

Sante
 
Kuna vitu vingi ambavyo hupelekea mama kukosa maziwa ya kutosha, sababu ya kwanza ni muda gani na mara ngapi kwa siku mama anatumia kumnyoshesha mtoto hapa huwa tunashauli mama awe anamnyonyesha mtoto mara nyingi zaidi usiku kuliko mchana kwana kichocheo kinachohusika na uzalishaji wa maziwa kwa usiku ndo kinakuwa active sana kuliko mchana, Pia sababu nyingine swala la kunyonyesha linahitaji utulivu na mazingira tulivu ili hisia ya mama iwe kwa mtoto ili kustimulate vichocheo na kutoa maziwa kwa wingi tatu kula sio Inshu but inategemea na vyakula anavyo tumia, kama utaweza tafuta mbegu za mamumunya saga vizuri tumia kwenye uji! lakin pia anaweza kupata ushauli mzuri zaidi pale klinik, Maana siku hizi kuna mfumo ambao unajulikana kwa jina la mama na mwana ipo chini ya wizara wanaweza kumuunganisha maana na huo mfumo akawa anapata elimu afya na ya lishe kwa ajili ya mtoto
 
Back
Top Bottom