Nini sababu ya msongamano wa watu hapa Busisi/Kamanga serikali ya awamu ya 6?

5991

New Member
Joined
Nov 26, 2017
Posts
2
Reaction score
1
Kuna kitu mie kinanitatiza sana jamani hivi kwenye utawala wa magufuli iwe ni Busisi au Kamanga, kwa kupitia vivuko hivi hivi tunavyoambiwa havitoshi sasa hivi mbona tulikuwa hatukalishwi kiasi hiki hapa kivukoni jamani, au ni mie tu naona hii shida?

Maana sidhani kama tatizo ni wingi wa vivuko shida ni matumizi ya hivi vivuko, idadi ni ile ile kama ya kipindi cha magu, ila ajabu sasa hivi ukiwahi kuvuka hapa sana umekaa masaa matatu au mawili na nusu, haya Kulikoni wadau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…