Twenty Twenty One
Member
- Nov 25, 2020
- 73
- 170
Ijumaa hii Simba ataanza kampeni yake ya kutinga robo fainali ya CAF CL kwa kumenyana na AS Vita Club ya DRC katika uwanja wa mashujaa pale Kinshasa. Pambano la mwisho uwanjani hapo alipoteza kwa 5–0 lakini mambo mengi yamebadilika katika vikosi vya timu zote mbili. Vita Club waliuza wachezaji wao hatari kama Francis Kazadi Kasengu, Fabrice Ngoma, Jean Jacques Makusu Mundele, Tuisila Kisinda n.k.
Simba wachezaji wa kikosi cha kwanza walioondoka ni wawili tu Emmanuel Okwi na kiungo mkabaji mghana lakini wakasajiliwa Tadeo Lwanga, Luís José Micquisson, Benard Morrison, Larry Bwalya, na Joash Achieng. Hawa wamedhihirika kuongeza ubora wa Simba. Pia wamemuongeza beki mzimbabwe Peter Muduhwa na striker mnaija Junior Lokosa. Hawa ubora wao haujafahamika bado ndani ya Simba.
Simba ya safari hii inaubora na uwezo wa kupata sare ama ushindi DRC na Sudan ikiwa watakuwa na utayari na ari ya kufanya hivyo. Lakini pia wanahitaji kufanya hivyo ili kujihakikishia nafasi mbili za juu. Msimu wa 2018-19 Simba licha ya kushinda mechi zake zote za nyumbani na kupata alama 9 bado ilihitaji wengine wamfanyie kazi na kweli Al Ahly alimfanyia kazi pale Algeria kwa kuwabana mbavu Saoura na kutoka nao sare.
Ilikuwa ni faida kwa Simba kwani kama Saoura angeshinda basi angemaliza na alama 10 na kufuzu huku Simba akibaki. Pia hao hao Saoura walimfanyia Simba kazi pale Kinshasa kwa kutoa sare ya 2-2 dhidi ya Vita club kwani Vita angeshinda basi angemaliza na alama 9 sawa na Simba lakini angemzidi Simba kwenye head-to-head, Vita alikuwa na magoli 6-2 hivyo angefuzu na kumwacha Simba.
Msimu huu hatuna uhakika kama El merrikh anaweza kufanya kazi hiyo pia hata hawa vita hatufahamu kama wanaweza kumzuia El merrickh (haijulikani yupi kati yao ni bora na anaubora kiasi gani) hivyo ni muhimu Simba akapata alama ugenini ili walau amalize na alama 13 yaani ashinde na kupata sare dhidi ya Vita na El merrikh (alama 4), kisha ashinde zote za nyumbani (alama 9).
Kwa kuzingatia ubora walionao na kutokuwepo mashabiki kwenye nchi hizo basi hili linawezekana kabisa. Hata hivyo wanapaswa kufahamu kuwa watajaribiwa sana kwa baadhi ya wachezaji kukutwa na covid-19 fake. Wawe na utayari wa mapambano.