Serendipity
JF-Expert Member
- Jan 24, 2009
- 486
- 43
Habari za leo wanjf,Leo ni sikukuu ya HALOOWEEN, naomba kufahamishwa tafsiri halisi ya neno HALOOWEEN kwa kiswahili, au maana yake kwa kiswahili tunaweza kufananisha na sherehe za mila ghani za kijadi kwa jamii yetu ya kitanzania?
Sasa unaposema bongo halloween kila siku, huku ni kuwa-insult wabongo!
Domenia na Tripo9 walau mmeweza kuonesha maana ya haloween japo bado inahitaji nyongeza ili kueleweka kinagaubaga, ila kwa ushauri wangu kwa muuliza swali yuko sahihi kwakuwa anapenda kufahamu, tatizo langu ni kwa wale wenzangu na mie ambao hawapendi kupitwa na mambo kama hawajui au wanajua wao ni kukurupuka na kutoa maana zinazopotosha na hata kudhalilisha yaani imeniuma sana mtu kusema bongo ni haloween kila siku?
natamani ningekuwa na uwezo nimpeleke akaone tukio husika alafu arudi na kubatilisha maandishi yake, ila kwa kifupi kwa ambao tuko huku leo mitaani hasa mida ya jioni mpaka usiku huu baadhi ya watu mitaani wamevaa vitu vya kutisha usoni, minguo ya ajabu ajabu yaani ilimradi wao wameadhimisha tukio husika, ila ukifuatilia kwa makini kuna programu ilikuwa ikionyeshwa live mimi kama mimi kwa maoni yangu ni upuuzi tena inadhalilisha wahusika waliokuwa wakishiriki tukio husika.
Kwa hiyo wakristo wameiga sikukuu ya kipagani na kuifanya yao?Haina maana kutafsiri "halloween" kwa sababu ni jina maalum.
Mfano: George Bush ni George Bush au unapenda kumwita "Mkulima Pori"? Hii ingekuwa tafsiri yake kwa sababu
a) "George" ni jina kutokana na neno la Kigiriki γεωργός = mkulima na
b) bush ni ama jina la aina ya eneo linaloitwa "pori" kwa Kiswahili (deep in the bush) au jina la miti midogo = kichaka
Kwa hiyo haina maana kutafsiri majina maalumu. Ila tu kile ambacho wanaJF wengine walieleza ni desturi ya Kimarekani iliyoanza kusambaa hata nje ya Marekani kutokana na filamu za kule zinazoanagliwa kote.
Siku yenyewe ya Haloween kiasili ni sikukuu ya kikatoliki ya "watakatifu wote" tarehe 1 Novemba ambako marehemu wanakumbukwa.
Eire walikuwa na desturi ya misa kwenye jioni kabla ya tar. 1. Novemba ("All Hallows' Eve" = evening before All Hallows = All Saints' Day -saint=hallow) na katika lahaja ya Eire ile "All Hallows' Eve" imekuwa "Halloween".
Ila tu desturi za kuvaa nguo za ajabu pamoja na vinyago si ya kale sana imejitokeza na kusambaa miaka ya nyuma tu.
Kwa hiyo wakristo wameiga sikukuu ya kipagani na kuifanya yao?
Tumekuelewa mkuu...!kuwa...Sielewi swali lako.
Katika nukuu yangu hakuna neno kuhusu desturi za kipagani. Kinyume chake nimeeleza ya kwamba jioni ya tar. 1. Novemba kuna uhusiano na sikukuu ya kikatoliki ya "Watakatifu wote" (All Saints).
Hali halisi ni kinyume cha kile unapolenga. Halloween ni mfano mzuri wa desturi mpya isiyo ya kikristo lakini ilijengwa juu ya msingi wa sikukuu ya kale ya kikristo (kikatoliki) katika nusu ya pili ya karne ya 20.
"Siku yenyewe ya Haloween kiasili ni sikukuu ya kikatoliki ya "watakatifu wote" tarehe 1 Novemba ambako marehemu wanakumbukwa."
Watanzania kwa kuvamia mambo ya USA basi nao eti nikasikia kuna Halloween Party hapa Dar!.................Yaani siku USA wakianzisha sikukuu ya kutembea uchi nahisi wabongo ndio watakuwa wa kwanza kuiga! Hovyo kabisa !!!