Nini tafsiri ya msemo "Mungu si Athuman"

Nini tafsiri ya msemo "Mungu si Athuman"

Tino Rushema

Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
5
Reaction score
2
Hi wana jf, naomba kuelimishwa maana kuna Usemi huu "Mungu si Athuman"siuelewi. Watu wanatumia huu usemi wanapofanikiwa ktk jambo flani ambalo hawakutalajia au kuwa na uhakika nalo.

Huyu Athuman alikuwa mtu wa namna gani kwenye maandiko?Kwanini awe yy tu asemwe si kama mungu kitabia asisemwe Ayub,Shaban,Hamis...........jibu kwa mwenye ufahamu.
 
Sidhani kwamba kuna athumani special anaenanishwa hapo. Athumani hapo na ni mtu (mchoyo)

After all huo ni msemo wa waswahili tu. Mataifa mengine hawatumii wala kumanisha Athumani huyo unaemuazia. (Not conclusive, just free thinking)
 
Mungu si Mashaxizo
 
Last edited by a moderator:
Maana yake Mungu si gaidi kama wenye dini anayosali athumani.
 
Maana yake Mungu si Mwanadamu, maana sisi wanadamu sometimes ni wachoyo au tunaupendeleo au kijicho, but Mungu hana hizo
 
Maana yake kwamba MUNGU SI BINADAMU. Hana choyo, wivu, upendeleo wala mapungufu yoyote...kikwetu tunasema 'Menya Enkai orgali'..maana yake ni sawa na hiyo hiyo.
 
Kwani athuman lina maanisha mtu mchoyo

Nooo! Athumani kwa hapo ni mtu tu. lakini mantiki ya msemo ni kwamba Mungu hana kinyongo. Coz sio mtu. Watu wote ni wachoyo tunatofautiana decree tu!
 
Maana yake Mungu si mwanadamu (Athumani huwakilisha mwanadamu).hii humtokea mtu anapopata nafasi nzuri ambapo aliiona haiwezekani mpaka atoe rushwa lakn hakutoa chochote na akapata hiyo nafasi.
 
hakuna aliyejibu swali mnazungukazunguka tu yeye anataka kujua over all names hapa duniani kwa nini likachukuliwa jina la athumani na sio lingine ,who was that athumani
 
hakuna aliyejibu swali mnazungukazunguka tu yeye anataka kujua over all names hapa duniani kwa nini likachukuliwa jina la athumani na sio lingine ,who was that athumani
-Alikua babu yangu
 
mungu hafananishwi na mwanadamu ambaye ana maamuzi ya kibinadamu. Athuman alikuwa miongoni mwa washika dini wa zamani ambaye alikuwa na nguvu ya kufanya miujiza mikubwa, pamoja na hayo lakini alikuwa hana uwezo kama wa MUNGU. Ndo maana watu humtaja Athuman kuwawakilsha wanadam wote kuwa hata iweje hawawezi kufanana na MUNGU kwa utendaji na maamuzi.
 
Back
Top Bottom