Nini tafsiri ya msemo "Mungu si Athuman"

hapo jina Athumani limetumika tu kama mwanadamu..hakuna preference yoyote katika uchaguzi wa jina hilo...na halihusiani na uchoyo tu..general idea ni kuwa Mungu hana tabia za kibinadamu (especially zile mbaya)
 
Maana yake Mungu si sawa na mwanadamu. Mungu ana upendo, ana huruma, ni msaada kwa kila mmoja bila ya kujali kabila, rangi, dini, au jinsia; tofauti na mwanadamu ambaye yeye huwa anaegemea sana kwa hayo niliyoayataja hapo juu.
 
hakuna aliyejibu swali mnazungukazunguka tu yeye anataka kujua over all names hapa duniani kwa nini likachukuliwa jina la athumani na sio lingine ,who was that athumani
Atakuja mwingine hapa na "ukimwona Zinduna na ambali yupo nyuma" na ataanza kuuliza huyu Zinduna ni nani hasa kwanini isiwe Rose au Asha, btw ni msemo tu kama ilivyo misemo mingine
 
Last edited by a moderator:
athuman ni mtu mfupi, mara nyingi hata watoto husema athuman mfupi yupo mlangoni wakimaanisha kufuli!
mtu mfupi hawezi kuona mbali bali waliomzunguuka! kwa kusema Mungu si Athuman maana yake Mungu si mfupi wa kuona karibu tu yaan wanaomzunguuka tu bali hata mimi wa mbali ameniona! Hivyo husema Mungu si Athuman! samahani kwa wamiliki wa hilo jina!
 
mPENDWA KWA HESHIMA NA taadhima nikujuze machache.. suali lako ni zuri na linatoa historiya !! Ni hivi...hadi kufikia karne 19/20 pwani afrika mashairiki ilikuwa ikitawaliwa na waarabu na lugha kiswahili ilikuwa ikiongewa kwa ufasaha...Pia Jina la OTHMANi (Athuman) ndo lilikuwa very very common ktk wenyeji wa humo.... (kwa vile swahaba Othman alikuwa mnyenyekevu na mtu wa watu katika Ennzi zake) jina hilo lilipendwa sana na wakazi wengi na kutumika katika mambo mengi na ktk biashara... kwa uaminifu wa mwenye jina.Hivyo ikapalekea jina la Athumani kuwa ni Mtu mema ila kasoro kuwa na Kudra iLaahia (Nguvu za kiMungu) !! ndo ukasikia "Mungu si Athumani"
 
Athuman ametajwa kama binadamu, siku zote wanadamu tuna madhaifu mengi, hatupendi wengine wapata mazuri kama Mungu anavyopenda sisi tupate mazuri. Mungu wetu ni mwema na anatupenda upendo wa kweli
 

Manaake Mungu si mwanadamu....matendo yake ni tofauti na wanadamu ni Mungu wa haki wala ahesabu makosa yetu hutoa ridhiki kwa kila mtu......
 
Kuna ingine naisikia HAMADI KIBINDONI..ila sijajua maana yake nini!
 
Baada ya enzi ya manabii na mitume kufikia hatma yao!! Bw. Athuman radhi za Moula zimfikie..kwa kuwa ndiye aliyekuwa mrithi wao " hivyo Athumani alikuwa mtu mwema,mkarimu,Mstahamilivu na Mwajibikaji na mwenye sifa za utu " Hadi kufikia utukufu huo ndipo ikapigwa methali hiyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…