Nini tofauti kati ya Mac book Pro na Mac book Air?

sanjomnyama

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2016
Posts
261
Reaction score
160
Wakuu habari za mchana,
Naomba kueleweshwa kwa mwenye kujua tofauti kati ya Mac book Pro na Mac book Air (apple) maana kuna jamaa kaniambia anayo na mimi nahitaji mac book so sijui ipi nzuri maana nashindwa nimuulize ni ipi kati ya izo ni nzuri au inaendana na wakati.Ahsanteni
 
pro kama jina lilivyo ina specs kubwa, imetengenezwa kwa ajili ya watu wenye matumizi makubwa kama video editors, graphics etc, na siku zote bei ni kubwa.

Air ni kwa ajili ya matumizi madogo kama mwanafunz, ofisini kwa mambo madogo na hata nyumbani kuperuzi na kucheki movie, bei yake huwa ndogo kuliko pro.

Yote hayo ni tisa, kumi inabidi ujue ni ya mwaka gani, hata kama ni pro kama ina core 2 duo ni bure itapitwa na air ya mwaka 2016 yenye core m, hivyo ni vyema kujua ni ya mwaka gani na specs zake.
 

Ahsante mkuu kwa hiyo nichukue ya mwaka gani sasa kama ni hiyo Mac Pro.??
 
kuanzia 2011 mwishoni, ila kuwa salama tafuta angalau ya 2012 ili kuepuka za 2011 mwanzoni. Na inavyokaribia 2017 ndio bora zaidi
Shukrani sana mkuu.., ngoja jamaa akileta niikague kwanza.
 
Ahsante mkuu kwa hiyo nichukue ya mwaka gani sasa kama ni hiyo Mac Pro.??

usisahau kitu kingine MacBook Pro nyingi Weight yake ni kubwa wakati Macbook Air ziko Slim na ni portable zaidi ila pia size MacBook Pro sana sana inaweza kuwa 15.6" au 13.3" wakati Macbook Air zinapatikana mpaka size ndogo zaidi 11.6".

MacBook Pro za nyuma kidogo mpaka 2011, nsijue hizi latest kuanzia 2015, zinakuja na HDD na mara nyingi ni 500GB HDD wakati MacBook Air mara nyingi zinakuja na SSD hii inafaida na hasara hapo hapo....Kwanza SSD ni very fast ukilinganisha na HDD lakini changamoto ya hizo MacBook Air utakuta SSD space nyingi zinacheza 128GB au 256GB na jinsi unavozidi kupanda juu size ya SSD bei inazidi kuwa kubwa sana.Hivo hii ni changamoto kama una Store mafile makubwa kwenye computer na kwa kifupi utahitaji External HDD ku supplement hiyo disk space ndogo.
Last but not least unaweza customize MacBook Pro mfano ukaiwekea SSD kama ilikuja na HDD lakini custimizations zinakua changamoto ukija katika ku Upgrade Macbook Air kwa upande wa Disk.

Inshort differences zake ni vigumu kuzichanganua kwa hapa iwapo hatuna real time example za computer mbili na mwaka zilipotengenezwa
 
Reactions: Ccc
Mac Air ni gharama chini kidogo kuliko mac pro.
 
Apple wamesitisha uzalishaji wa generation ya mackbook air, ya mwisho kabisa kuzalishwa ni ya mwaka 2015. Kwa sasa wameirudisha mackbook kuireplace mackbook air.
Mackbook ni nyembamba zaidi na ina kioo kizuri zaidi kama cha pro. Imetoka kwa 12 inc ila haina nguvu ukilinganisha na air kuanzia processor mpaka perfomance.
Ni kama ipad iliyoongezewa keyboard tu na inauzwa ghali zaidi.
 
mkuu,naomba kujua advantage za kumiliki iMAC au ina sifa gani kama umewahi kutumia maana nafikilia kununua


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu imac advantage yake ni kwamba ina kioo hapo hapo, desktop na monitor vimeunganishwa.
Kuhusu mambo mengine kama processor/ram/hdd unaangalia kama vifaa vyengine. Ungeeka model husika na kiasi cha bei ingekuwa vizuri kushauri zaidi.
 
Mkuu imac advantage yake ni kwamba ina kioo hapo hapo, desktop na monitor vimeunganishwa.
Kuhusu mambo mengine kama processor/ram/hdd unaangalia kama vifaa vyengine. Ungeeka model husika na kiasi cha bei ingekuwa vizuri kushauri zaidi.
hii inaweza kufanya kazi kama pc nyingine za window,au ina mipaka kama zilivyo simu zao???

i mean kuingiza nyimbo,kusoma flash na kiweka nyimbo nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Habari!
Naomba nisaidie nunatumia Mac book Air lakini imekuwa na tatizo la kuzimika ghafla hasa charge inapofika 75% ni takribani miezi miwili sasa. Mwanzo ilikuwa inazima chaji ikiwa 34-35%.
Na huchaji mpaka ifike 100% ndio huitoa katika chaja yake.
 
Mara nyingi mkuu hii hutokana na battery kuanza kufa, na sio macbook tu vifaa vingi vinavyotumia battery huweza kupata tatizo kama hili.

Pia nimecheki online kuliwahi kuwa na firmware issue inayosababisha hili tatizo na solution yake ni ku update Mac yako kwenda latest version. Hivyo angalia kama unarun latest version.
 
Wazee vipi kuhusu MacBook Retina Inch 12 ya 2016.
Processor: 1.2GHZ dual core intel core m5.
Memory: 8gb 1867 MHZ LPDDR3
Graphics: Intel HD graphics 515 1536 MB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…