Alejandroz
JF-Expert Member
- Feb 14, 2017
- 329
- 413
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanakuja mkuu usiende mbali
[emoji1374]Jaji ni mwamuzi wa kesi katika mahakama kuu. Cheo chake ni cha kuteulowa na raisi na anasimamia sheria za uamuzi zinazotumika katika mahakama kuu.
Hakimu ni mwamuzi wa masuala na kesi zinazowasilishwa katika mahakama ya mwanzo, wilaya na ya hakimu mkazi mkoa. Mamlaka yao huyapata kwa kuomba kazi na kuajiriwa na kama watumishi wengine wa serikali. Kwa ngazi ya kimamlaka suala likishidikana mahakama za chini zinazosimamiwa na mahakimu basi anayeona hajaridhishwa na huo uamuzi wao atakata rufaa kwenda kwa jaji.
Kuna masuala hutakiwa kuanzia kwa mahakimu na pia kuna masuala ni lazma yaanzie kwa jaji(mahakama kuu).
Nashukuru kwa elimu hiiHawa ni watu wawili wanaofanya kazi moja ya kuhukumu kesi mahakamani.
Utofauti wao ni kwamba;
1. Level: Hakimu ni kuanzia mahakama za mwanzo, wilaya na mahakama ya mkoa wakati jaji ni kuanzia mahakama za juu yaani mahakama kuu na mahakama ya rufaa ambayo ndiyo mahakama ya mwisho katika kutoa maamuzi nchini.
2. Upatikanaji wao: Hakimu anapata kazi kwa kuomba kazi utumishi na kuajiriwa wakati jaji anapatikana kwa kuteuliwa na raisi pekee kwa kigezo cha kufanya kazi za kisheria (hakimu, wakili n.k) kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo na kuendelea.
3. Kuwafukuza kazi: Ni rahisi kumtimua kazi hakimu lakini kwa jaji hali ni tofauti hata kwa raisi mwenyewe. Maana inabidi raisi aunde tume ya majaji toka jumuiya ya madola ndio watoe mapendekezo juu ya makosa yake.
Jaji (judge), hakimu (magistrate).Nijuavyo mimi,
Jaji "Judge" ni kwa lugha ya Kiingereza,ni sawa na tunavyosema Shati "Shirt" Hakimu ni neno la kiarabu "Hakam" mtu anayehukumu.
Mahakama ya Rufani je??Jaji ni mwamuzi wa kesi katika mahakama kuu. Cheo chake ni cha kuteulowa na raisi na anasimamia sheria za uamuzi zinazotumika katika mahakama kuu.
Hakimu ni mwamuzi wa masuala na kesi zinazowasilishwa katika mahakama ya mwanzo, wilaya na ya hakimu mkazi mkoa. Mamlaka yao huyapata kwa kuomba kazi na kuajiriwa na kama watumishi wengine wa serikali. Kwa ngazi ya kimamlaka suala likishidikana mahakama za chini zinazosimamiwa na mahakimu basi anayeona hajaridhishwa na huo uamuzi wao atakata rufaa kwenda kwa jaji.
Kuna masuala hutakiwa kuanzia kwa mahakimu na pia kuna masuala ni lazma yaanzie kwa jaji(mahakama kuu).
Prosecutor ni mwendesha mashitaka, mfano Serikali inapomshitaki mtu/ taasisi.Prosecutor
Counsel
Plantiff
Hawa ni kazi zao ni zipi
Kwa hiyo mahakama kuu hazina mahakimu?Jaji (judge), hakimu (magistrate).
Tofauti yao ni mahakama wanazohudumu, jaji akiwa mahakama za juu iwe ni ya mkoa, Kuu au ya rufani. Hakimu ni kwa mahakama za chini, mfano ya mwanzo, ya wilaya.
Unaweza peleleza kwenye tovuti yao.Kwa hiyo mahakama kuu hazina mahakimu?