Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
Ni maneno mawili yanayochanganya sana,ikitokea mtu anasema ukweli anaambiwa ni mchochezi/anakashifu.Mfano Gazeti la Mwanahalisi.mpaka likafungiwa kwa kile kinachodaiwa uchochezi.Kwa hiyo serikali au mtu akikosea asiambiwe ukweli kwa kuwa ukweli unageuzwa kuwa uchochochezi?Waislamu siku zote wamekuwa wakiiambia serikali ukweli,wanakuja na tuhuma kuwa hawa watu ni wachochezi.Nataka anayejua aelezi nini tofauti ya ukweli na uchochezi.
Najua ukweli siku zote unauma,na watawala siku zote hawataki kuambiwa ukweli.Lakini tukae tukijua ukweli pekee ndio humuweka mtu huru.Tukiambiana ukweli uovu na ufisadi hautakuwepo,watu wataheshimiana na amani itatamalaki nchini kwetu.
Tukiendelea kuwashutumu wanaotuambia ukweli hatutafika.Dawa kujirekebisha.
Naipenda nchi yangu Tanzania.