Kiburi ni Hali ya mtu kuwa na Aina fulani ya dharau lakini Mara nyingi inakuwa ndani kwa ndani. Inaweza kuwa mtu hasalimii au akitumwa haendi na akiulizwa anakaa kimya hajibu kitu. Sio lazima aseme ila matendo yake yanaonesha dharau
Jeuri sasa ndio kiboko. Mtu hajali na anaonesha dharau wazi wazi na anatamka kabisa. Mtu anakuwa na uwezo wa kukufanya kitu chochote hata kama ni cha kukuumiza kwa makusudi lakini huwezi kumfanya kitu. Hii inakuwa inalindwa na nguvu kutoka nje ya huyo mtu. Yaweza kuwa ana nguvu ya ziada sababu anatumia hela zake kuwahonga walinda usalama au walinda sheria, yaweza kuwa anatumia cheo chake katika jamii kutokufanywa kitu au urafiki wake/undugu wake na wanaotakiwa kumshughulikia
Katika summary, kiburi ni tabia/nguvu iliyo ndani ya mtu hata akiwa mnyonge vipi ila Jeuri Mara nyingi inaletwa na nguvu au Hali kutoka nje ya mtu