Nini tofauti ya msomi na asiye msomi?

Kusoma hakumuondolei mtu upumbavu kuna kusoma na kuelimika wengi wamesoma Ila hawajeelimika hujawai kumuona msomi anaweka vidore puani tena bila kitambaa anachokonoa uchafu?
 
Then ukipata maarifa ujinga unaisha?

Kuna wadau wamesema huko juu ujinga unaweza kuondoka ila upumbavu kuisha ni kasheshe
Ujinga hauishi
Kitendo cha kutojua baadhi ya mambo kinakufanya uwe mjinga. Na haiwezekani ukawa unajua kila kitu.
 
Elimu ya vyeti sio?
Msomi ni mtu yoyote aliyesoma akatunukiwa cheti Lakini haimaanishi kwamba ana akili, akili ni Kitu kingine kabisa kwanza akili haina mipaka Lakini pili mabeberu walitumia akili nyingi kuweka elimu ili msijitambue wawatawale kiurahisi ELIMU ni mfumo mbovu wa kwanza alafu unaofuatia DINI alafu AFYA.
 
Msomi ni mtu yoyote aliyesoma akatunukiwa cheti Lakini haimaanishi kwamba ana akili akili ni Kitu kingine kabisa kwanza akili haina mipaka
sawa
Lakini pili mabeberu walitumia akili nyingi kuweka elimu ili msijitambue wawatawale kiurahisi ELIMU ni mfumo mbovu wa kwanza alafu unaofuatia DINI alafu AFYA.
Hebu fafanua ki vipi elimu imekua mfumo mbovu kwetu

Elimu imetumika vp sisi kutawaliwa kirahisi?

Hapo kwenye dini na afya tutaendelea
 
Kila mtu ni mjinga kwa wakati wake,ujinga huondoka baada ya kulijua jambo ambalo ulikua hulijui,unaweza ukawa Pilot ila ukawa mjinga kwenye kutengeneza Baiskeli.
Huenda, narudia tena neno "huenda" msomi kuanzia shahada kwenda juu, chini ya hapo sio msomi.
 
sawa

Hebu fafanua ki vipi elimu imekua mfumo mbovu kwetu

Elimu imetumika vp sisi kutawaliwa kirahisi?

Hapo kwenye dini na afya tutaendelea
Utumwa unakuja pale ambapo unatunukiwa cheti maana yake uajiriwe na lazima uwe na cheti kuthibitisha elimu yako huo ni UTUMWA mwanzilishi wa hii platform Maxence Mello hategemei cheti kama nilivyosema hapo awali akili haina mipaka na hakuna binadamu aliyeweza kuitumia akili yake to the maximum mabeberu wanalitambua hili ndo maana wakaweka ELiMU Lakini labda nikuulize swali dogo tu ivi elimu ndo mafanikio au elimu ndo ufunguo wa maisha?
 
Asante sana
Elimu inaweza kukusaidia kufikia mafanikio yako kwa urahisi zaidi

Mf: ukasomea udaktari elimu hiyo itakupa ajira na mwisho kipato kwa urahisi zaidi na mwisho kufikia mafanikio yako unayotaka

Maxnce mello huenda elimu yake ilichangia pakubwa kuweza kufungua kufungua hii platform

We unadhani angefunguaje platform kama hii bila kujifunza namna ya kuiendesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…