Nini tofauti ya neno bahari na pwani, pls.

Nini tofauti ya neno bahari na pwani, pls.

Angel Nylon

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
9,164
Reaction score
18,402
Jee ni maneno tofauti yenye maana 1 au kila moja lina maana yake?
Km kuna tofauti ktk maana naomba kujua tafadhali
 
jamani angel....mbona bahari ni kwenye maji na pwani ni nchi kavu pembeni ya bahari....au nimekosea....?
 
Pinda anajua sana haya mambo msubiri atakuja sasa hivi kukujibu
 
jamani angel....mbona bahari ni kwenye maji na pwani ni nchi kavu pembeni ya bahari....au nimekosea....?

Upo sahihi kabisa mkuu, bahari ni eneo lote la maji na pwani ni eneo la nchi kavu lililo mkabala na bahari yaani eneo la ardhi kavu kuanzia pale maji yanapoishi. Kisheria wanasema ni mita 60 toka eneo la mwisho kabisa la bahari kuelekea nchi kavu.
 
pwani ni eneo la nchi kavu lililo mkabala na bahari yaani eneo la ardhi kavu kuanzia pale maji yanapoishi. Kisheria wanasema ni mita 60 toka eneo la mwisho kabisa la bahari kuelekea nchi kavu.[/QUOTE said:
wewe nafikiri unamaanisha UFUKWENI au Beach.

pwani ni ukanda agharabu ni kilomita kadhaa kutoka mwisho(mpaka wa bahari na nchi kavu) , ndio maaana Dar, kibaha, kisalawe, tanga, mtwara mikindani hili ni eneo la pwani = costal. enzi zile za kina said barghash mwarabu aliyeiharibu Zanzibar alijimilikisha kilomita kadha za ukanda mzima wa bahari Hindi kutoka Ramu kenya mpaka msumbiji
 
Asanteni kwa majibu, mi haya maneno yalikua yananibabaisha kusema kweli, nlijua kando kando ya bahari ni ufukwe na si pwani, sasa nkawa najiuliza hii pwani ndo nn? Au ni bahari + ufukwe?
Nimefahamikiwa, shukran
 
Ufukweni- sehemu ya mchanga ambapo maji hukutana na mchanga.
1-Pwani - sehemu ambapo maji yake hayana kilindi kikubwa, ni kusema maili kadhaa kutoka ufukweni.
2-Pwani / Mrima/ Mwambao - maeneo / miji ambayo hayako mbali sana au hupakana na Pwani
Bahari- sehemu ambayo maji yake ni ya kilindi kikubwa.

wajuzi tujuzeni
 
bahari ni eneo la maji (zaidi ya maziwa na mito) ukubwa wake umeeneea sehemu mbali mbali na kufanya umbo moja la maji japo baadhi ya sehemu litapewa jina tofauti.
Fukwe ni sehemu ya nchi inayopata athari ya moja kwa moja kutoka baharini.
Pwani ni eneo lote lililo karibu ya bahari ambapo limepata athari za muda mrefu kutokana na uwepo wa bahari-hali ya hewa ,uoto wa asili nk
 
pia naona hilo ni jibu sahihi
 
Tofauti ya bahari ni ya dunia nzima ila pwani ni ile iliopo karibu nawe
 
Back
Top Bottom