Asante kwa maelezo ya kina,ila bado sijelewa kwanini sentensi yangu ya kwanza ina makosa kwa sababu umetoa tafsiri ya
Vuma³: enda kwa kupita Haraka
maana yake hicho ni kitenzi hivyo kusema
Wanajeshi 'walivuma' makombora maana yake waliyarusha/kufanya yaende kwa kupita haraka.
Ukisema makombora yalivuma
maana yake umetumia tafsiri uliyotoa mwenyewe namba 1,ambapo umesema
Vuma¹: toa sauti nzito,mfano upepo,ngoma, nyuki, maji
Hapo maana yake makombora yalitoa sauti nzito kama upepo,ngoma nk
Hivyo naamini sentensi yangu ya kwanza ipo sahihi ukitumia tafsiri ya tatu na pia sentensi yako ipo sahihi ukitumia tafsiri ya kwanza.
Sent using
Jamii Forums mobile app