Unajua Xtrail ni moja kati ya gari chache za Kijapan zinazouzwa Ulaya. Huko jamaa wako makini saana na running costs za magari, tofauti na Marekani. Sasa kikubwa kwenye diesel engines ni matumizi madogo ya mafuta, pia diesel ni cheap kuliko petrol, na kikubwa ni kwamba, diesel in torque kubwa (nguvu ya kusukuma gari) kuliko petrol. Diesel ina balaa lake. Engine za diesel mara nyingi zina kelele kuliko za petrol, na wakati wingine zinakuwa na vibrations nyingi zaidi. Na pia zina tabia ya kusumbua pale gari linapokuwa na high mileage, hasa kama ni turbocharged.
Engine ya petrol inatumia mafuta mengi kidogo kulinganisha na diesel, na pia ni gharama kununua petrol kuliko diesel. Ila ina faida nyingi pia. Gari petrol linakuwa na horsepower kubwa (hii ni nguvu inayoliwezesha gari kwenda kasi) kuliko diesel. Utasikia watu wakisema petrol inachangaya haraka kuliko diesel, ila diesel ina nguvu kwenye mlima. Ni vile kwenye mlima torque ndio inahitajika zaidi.
Ila kwa kuwa sisi tunanunua gari used, nashauri petrol zaidi kuliko diesel kwa hizo gari ndogo. Na pia, spare za diesel cars ndogo ndogo sio nyingi kama za petrol