Nini tofauti ya Petty cash, Cash sale, Invoice, Receipt na proforma?

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Jamani mwenye kujua maana ya hivi vitu na jinsi/wakati gani vinakuwa applicable na kipi kinaanza na kufuatia anijulishe:
Petty Cash book/Voucher
Cash Sale
Proforma Invoice
Receipt
na nyingine unazozifahamu.

karibu.
 
Petty cash ni cash inayotengwa na ofisi kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya ofisi,cash sale mauzo yanayofanyika kwa kulipa fedha taslim na si kwa mkopo,,proforma invoice ni document inayoandikwa wakat unaenda kuuliza bei za vitu fulani,,kabla kufanya manunuzi,mara nyingi unaandikiwa km unataka kufanya quotation za bei kwa kifaa unachotaka kununua yaan unashindanisha bei ya kitu kimoja zaidi ya maduka mawili ili kupata uafadhali wa bei,receipt ni stakabadhi kwa maana ya karatasi maalumu unayopewa mara baada ya kufanya manunuzi lakini umeyalipia iwe ni cash au hundi
 
Na kuna kingine kinaitwa tax invoice,document unayopewa mara baada ya kuandikiwa proforma then ukakubaliana na zile bei then unataka kununua vile vitu but kwa mkopo mara nyingi na malipo hufanyika kwa cheque (si mara zote),,,na kuna kitu kinaitwa delivery note,,ni document inayoonyesha idadi ya vitu ulivyonunua na acknowledgement ya mnunuzi kuwa amevipokea na vipo sawa
 
Petty cash ni ushahidi wa mpekeaji na mtoaji wa hela taslimu kupokeewa na muhusika ndio maana kuna sehemu za signature za wote wawili, Cash sale ni malipo ya mauzo yaliyouzwa kwa pesa taslim, proforma invoice inatumika kama kielelezo cha bidhaa zinazohitajiwa pamoja na bei zake, hutolewa kwa mtu anaetaka kufanya manunuzi kuipeleka ofisini ili iweze julikana bei za bidhaa na kiasi cha pesa kinachotakiwa kulipwa, na hailazimishi aliepewa proforma invoice kuja kufanya manunuzi kwa duka lilotoa hiyo proforma, muhusika anaweza pitia sehemu tofauti na kupokea proforma ili aweze linganisha bei ubora wa bidhaa na terms za malipo, erceipt hutolewa baada ya kukamilisha malipo iwe kwa cash, au cheque. Hivi ndivyo ninvyoelewa nasubiri mawazo ya wengine pia.
 
Proforma Invoice - ni mchakato wa kutafuta 10%. Ha ha ha!
 
kote ni sawa lakini hapo kwenye red umechemsha jibu ni lile alilolitoa Mariam Edward
Petty cash ni cash inayotengwa na ofisi kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya ofisi,cash
 

kwenye petty cash umejichanganya kidogo. hayo maelezo ya mchangiaji hapo juu yamekaa vizuri zaidi.
 
Petty Cash
Hii ni Cash kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya kiofisi kama Chai, sukari, majani ya chai, printer catridge, stapler pin, etc.

Cash Sale,
Haya ni mauzo yanayofanyika kwa fedha taslim, hakuna mkopo hapa.

Proforma Invoice
Hii huitwa pia QUOTATION. Ni document inayoandaliwa na muuzaji ili kwenda kwa mnunuzi mtarajiwa ikielezea nia ya muuzaji ya kumuuzia mnunuzi mtarajiwa bidhaa mbalimbali kwa bei husika. Mara nyingi mnunuzi mtarajiwa ndio hua anamuomba mnunuaji amuandalie hii document ili yeye aende akafanye maamuzi (labda) baada ya kuzipitia hizi kutoka kwa wauzaji wengine mbalimbali.

Receipt,
Hii documents anayoandaa muuzaji kwenda kwa mnunuaji ikionyesha kua bidhaa iliyonunuliwa tayari imelipiwa na haidaiwi.

Invoice,
Hii ni document ambayo huandaliwa na Muuzaji kuonyesha kua mauzo yamefanyika tayari (iwe cash au mkopo). Kama ni mkopo basi hutumika pia kupelekewa Mnunuaji kama kithibitisho kua anadaiwa. Invoice sanasana ziko za aina mbili kuu.

Tax Invoice
Hii ni document anayoandaa muuzaji kwenda kwa mnunuaji ikionyesha kua mnunuaji amenunua mzigo fulani kwa bei husika. Na hii Tax Invoice inamaanisha mzigo huo umechajiwa kodi ya VAT

Sales Invoice
Hii ni kama hiyo hapo juu, ila tofauti tu ni kua mzigo wa category hii hua hauna kodi ya VAT

Delivery Note
Hii document anayoandaa muzaji kwenda kwa mnunuaji ili mnunuaji aisaini pale anapopokea mzigo. Mara nyingi mnunuaji akishasaini basi copy (au original) ya hii hurudi kwa muuzaji. Hii mara nyingi hutokea kwa watu wanaofanya biashara kwa mkopo. Muuzaji anatakiwa kumthibitishia mnunuaji kua alipokea mzigo hivyo huambatanisha hii DN kwenye invoice ili mnunuaji asipate tabu ya kuanza kukumbuka kama alipokea au lah.

Goods Received Note
Hii ni.document ambayo huandaliwa na upande wa Mnunuaji, hususan watu wanaotunza mzigo(store) kuonyesha kua ni kweli wamepokea mzigo ukiwa kamili kama ulivyotumwa. Na kama kuna upungufu basi wanatakiwa wauonyeshe.
 

Great mariam, can u put it English please!
 

we mtoto utakuwa ulikuwa unakimbiza sana class yaani umetoa maelezo sawia kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…