The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 10,805
- 14,181
Siku hizi wakweli wanaitwa wambea ,na wambea wanaitwa wakweli ,maana kuna jamaa hapa mtaani akikuona umeoa na unamchepuko basi lazima akuite na kukukanya uache tabia ya kuchepuka ,majuzi kuna dada mmoja rafiki yangu alitoka na mchepuko wake beach wakawa wanashikana shikana jamaa akawaona kesho yake akamfata huyo dada na kumuonya ,sasa yule dada akanifata kuniambia jamaa hawezi mwambia mumewe nikamwambia hata mimi alishawahi nikuta huwa mlokole yeye anafikiri anatimiza wajibu kumbe ukweli watu hatuwezi badilika overnight pia nikamuhakikishia hawezi mwambia mumewe,sasa cha ajabu hapa mtaani jina lake la siri ni chaumbea ,mi naona ni chaukweli anayefuatilia yasiyo yake,umbea ni kusema jambo ulilotegemewa utalificha angekuwa anawambia wanaoibiwa huo ndo umbea.