Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kutokana na hali ya kiuchumi ya dunia na mwitiko wa nchi tajiri kukabiri hali hizo ni wazi kuwa kuna vitu ambavyo serikali inapaswa kuvifanya na kutoviacha soko huru. Mwaka 1967, tulitangaza azimio la Arusha na kutaifisha (kuviweka kwenye himaya ya serikali) vitu vingi. Baadaye miaka ya tisini vitu hivyo vingi vilianza kurudishwa kwa wananchi katika kile kinachoitwa ubinafsishaji.
Mabenki, Bima, makampuni ya uzalishaji n.k yakaanza kuuzwa na kuondolewa mikononi mwa serikali. Leo hii hali ya uchumi ya dunia inatufanya tuhoji je kuna vitu ambavyo tuviweke moja kwa moja mikononi mwa serikali, na ni vitu gani hivyo na kwa nini? Na ni vitu gani ambavyo vinaweza kuwa bado chini ya watu binafsi lakini serikali ikiwa na hisa za kikamkakati (strategic shares) kama UK kwenye BAE na nchi nyingine?