Nini uzuri na ubaya wa vigae vinavyoundwa na wakala wa ujenzi?

Nteko Vano

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
434
Reaction score
111
Wana JF

Katika pitapita yangu nikakutana na waheshimiwa wa wakala wa ujenzi na vigae vya kuezekea nyumba. Vigae hivi ni bei nafuu na inawezekana vikawa mkombozi kwa mtanzania, kigae kimoja ni sh 350/= na kwa nyumba kubwa self ya vyumba vitatu hadi 4 vigae takribani 2000 hadi 2500 vinahitajika. Unaweza ukaezeka kwa laki 7 hapo.

Je, ubora wa vigae hivi ukoje? Kwa wale wenye uzoefu na vigae hivi naomba tupeane ushauri.

Nawasilisha.
 

Wakala WA ujenzi wanapatikana sehemu gani mwanza wapo
 
wapo dar pale mwenge sam nujoma karibu ka hospital ya jeshi
wanaitwa national housing and building research agency
jaribu pia kutembelea wavuti yao

mimi nipo mwanza sitakuwa tena ishu ya kusafirisha kwani mikoani hawana matawi
 
kwani mkuu vigae vingine vinauzwaje?
 
Hukufanikiwa kupiga ka picha?? Ni vigae vya clay, au bati??
Alaf ulivyo sema wakala wa ujenzi nikajua TBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…