Vipaumbele vya awamu ya sita ni kumalizia miradi yote ya awamu ya tano ili isiishie njiani na kubakia magofu.
Kipaumbele cha pili ni kuwa rafiki na jumuiya ya kimataifa, ndio maana Mulamula akapewa nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje ili uzoefu wake urudishe uhusiano mwema na mataifa haswa yale makubwa duniani.
Kipaumbele cha tatu ni kuhakikisha nchi nzima inapata maji, miradi mikubwa inafunguliwa miaka ya sasa.
Huo ni mueleko tosha kabisa. Kikao kama kile cha COP26 kuhudhuriwa na rais mwenyewe ni sehemu tu ya umakini wa muelekeo mzima wa awamu ya sita.