Ninunue desktop computer yenye specifications gani ili baadae ni upgrade mwenyewe?

Core 6 thread 12

Sema zipo core i7 na i9 zenye core 8 pia,

I7 8700 core 6
I7 9700 core 8
Hivi mkuu ninaweza kuupgrade desktop core i3 generation ya 8 kwenda core i7 generation ya 8 au kwenda core i9 generation ya 8?
 
Mkuu Chief Mkwawa ahsante sana kwa muda wako na ushauri.
 
Natumae mleta mada umepata muongozo...
Bila shaka mkuu nimepata mwongozo wa kutosha na niwashukuru wana JF bila kujali umri, rangi, cheo, ujuzi, uzoefu pamoja na dini. Nilikuwa nipo njia panda kwa kipindi sasa, lakini kwasasa nategemea kuwa na mashine yenye akili kubwa kuchakata data. Na hii ni kutokana na uhitaji wangu na bajeti finyu.

Mwisho wa mwezi huu nitaingia Dar hapo kuzunguka machimbo ambayo nimeelekezwa pamoja na kuwasiliana na baadhi ya wadau ili kufanikisha ununuzi wa hivyo vitendea kazi.

Ninaamini uwepo wenu hapa JF si bure na muendele na moyo wa Kujitoa kwani wengine bado baadhi ya mambo tuomba ufafanuzi kwenu ninyi qenye upeo kwa kiasi chake.
 
Habari ndugu #chief mkwawa kwa mchango wako.

MREJESHO

Nilifanikiwa kununua Desktop yenye specs hizi hapa:

INTEL PENTIUM DUAL CORE E5700 3.0 GHZ, RAM 2GB, 320HDD BRAND HP.
WAT 65.

Naomba #CHIEF MKWAWA uniambie je kwa ushauri wako nitaweza kuiup grade hiyo mashine??? Na je ni generation ya ngapi? Mana nimeyumba sana kariakoo na duka ulilonitajia niliambiwa hawana kwa sasa. Niliipatia duka moja mtaa wa msimbazi B kariakoo kwa bei ya 160k.

Bado sijaijua gen ya ngapi na nikii upgrade nifanyaje. Karibuni wadau. Asanteni kwa michango yenu.
 
Dah mkuu hii wame kupiga, huwezi kuirudisha? Hii ni Pentium ya zamani sana, una upgrade kwenda core 2 duo.

Kaale mbona nilikwenda karibuni zipo machine bado?

Pia naona kupatana/zoom Tanzania pentium za 6th gen za kutosha around 180,000.
 
Dah mkuu hii wame kupiga, huwezi kuirudisha? Hii ni Pentium ya zamani sana, una upgrade kwenda core 2 duo.

Kaale mbona nilikwenda karibuni zipo machine bado?

Pia naona kupatana/zoom Tanzania pentium za 6th gen za kutosha around 180,000.
Aiseee kumbee. Kaale nimefika nimeeuliza wanasema hawana tena. Anyway basi tena nipo mkoani ngoja niitumie kwa kazi nyepesi tu nitafanya mpango tena. Ila kaale nilifika boss.

Kaz bado ninayo Kumbe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…