Kila siku kualika watu waje kwenye makutaniko yenu ili wapate miujiza ya uponyaji. Slogan zenu za WAGONJWA WATAOMBEWA nataka muonyeshe kama kweli huyo Yesu Kristo anatenda kazi pamoja na ninyi basi: 1. Fufueni wafu 2. Waponyeni amputees ( watu waliokatwa miguu au mikono). Msilete hadithi za kuponya kisukari, ukimwi,kansa, ugumba etc. Hayo mawili nimewapa mtihani. Mkishindwa nawashauri wafuasi waachane nanyi. Kama mna hoja yoyote leteni hapa niijibu. Nataka taifa langu liamke usingizini na kuachana na haya matapeli ya miujiza feki.