Nioe Kabila gani?

Kabila lolote na ukitaka taifa lolote.ili mradi muwe na mapenzi ya dhati na uridhike.
 
Hauoi kabila mkuu unaoa mtu/binadamu-kabila ni kama jina tuu/utambulisho
 
Nioe kabila gani?
Haya mambo ya makabila mbona tunayapa nafasi? Tz hayana nafasi haya labda nchi za wenzetu. ANYWAY, oa kabila lako, ukikosa, oa kabila langu,pia ukikosa oa popote kabila si issue.Binasfi mambo ya ukabila kabila sipendi.
 
mi nadhani oa mtanzania, kuhusu kabila watanzania swala la ukabila hatuhitaji kuliangalia sana..cha muhimu ni upendo wa dhati....kama ungeuliza uoe nchi gani hapo ningejaribu kukushauri ila na hapo pia binadamu wote ni sawa tunatofautiana tabia tu mkuu...oa uliyeona anakufaa
 
Mkuu siku hizi kama mwanamke ana haja ya kuolewa na kujiheshimu na anapenda kuishi kwenye ndoa, hakuna cha kabila wala nini, ukifuata makabila utaula wa chuya baba, penda unapopendwa. kuna watu wanajuta mpaka leo, walipendwa na wasichana wasio wa makabila ya kwao, lkn wazazi wao wakalazimisha wakaowe kabila lao, basi maisha si yale tena, daily mtu ana complain maana hakukuwa na mapenzi pale bali kuridhisha wazazi tu. mimi sijaoa kabila langu na wala sioni tofauti yeyote ni raha tupu
 
Nioe binti wa kabila gani?

ICU, kuongea mambo ya kabila kunakera baadhi ya watu na mimi ni mmoja wao. Una maana gani kuongelea kabila wakati wewe unatafuta mke? Kwani baada ya kuoana unataka kuanzisha matambiko ya kikabila? Binafsi nakereka sana na mambo ya kabila na ukabila.

Mimi nilimwoa mtu ambaye alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na sasa ni rafiki mzuri na mke wangu tunayependena sana. Sijui kama ningepata mke wa namna hii kama kweli ningeendekeza mambo ya kabila. 😕😕
 
Unajua nimeuliza hivi kutokana na thread moja hapa hapa jukwaani inayozungumzia udhaifu wa makabila fulani
 
DC, Samahani mkubwa, nimekuelewa, hongera kwa ndoa yenye amani na upendo
 
Haya mambo ya makabila mbona tunayapa nafasi? Tz hayana nafasi haya labda nchi za wenzetu. ANYWAY, oa kabila lako, ukikosa, oa kabila langu,pia ukikosa oa popote kabila si issue.Binasfi mambo ya ukabila kabila sipendi.
tall, samahani kwa kukukwaza ila ndio najifunza kwani may be nilikuwa ICU kwa kufikiri ukabila kumbe sio tija
 
Preta, asante Ndugu
 
Unajua nimeuliza hivi kutokana na thread moja hapa hapa jukwaani inayozungumzia udhaifu wa makabila fulani

Achana na huo upuuzi. Kama umempata mtu anayekupenda na wewe unampenda mshukuru Mungu na kusonga mbele. Ukianza kuangali mambo ya hovyo kama hayo unaweza kujuta maisha yako yote. Hebu soma maelezo ya Mkuu Chimunguru hapo chini.

 
kabila lolote linafaa mradi yuko kimaadili ya ndoa zaidi !
 
Karne hii bado unajiuliza uoe kabila gani???
 
Karne hii bado unajiuliza uoe kabila gani???
bht dada, kwani nimekosea kuuliza? unajua karne wazee wanasema haiondoi asili, ila hapa nimeanza kujifunza sasa
 
LK, ndio nauliza siwezi kusema nataka kabila gani kwani am totally blind on this

Usijali ICU, hapa ni kutenda miujiza kwa watu blind kama wewe. Hesabu tatizo lako limekwisha. Oa mhaya, mzanaki, mchaga au kutoka makabila yote matatu. Zingatia ushauri huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…