Niolewe na nani mie!

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,378
Reaction score
3,383
Mke asiye na mume, akamchumbie nani?

Isingekuwa vigeni, mwanamke kuchumbia
Ningepita mitaani, mume kujitafutia,
Nisimuudhi Manani, ndio nimejizuia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Ndege maingainga, si jambo la kujitakia,
Mume mwema natamani, vipi tajitafutia?
Na mwanamume haini, sitaki kunichumbia,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Nimetulia nyumbani, sina mume kunioa,
Wanifuatao ndani, si wachumba wa kuoa,
Hutaka kunirubuni, maasini kunitia,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Ndege maingainga, si kosa langu sikia,
Niliolewa zamani na mume mwenye udhia,
Kanitia kilabuni, pombe kumchuuzia
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Mimi nikamuamini, huku machozi nalia,
Mume hii kazi gani, alokataza jalia?
Kheri tukate kuni, mimi nitakuuzia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Akapanda hasirani, na maneno akafyoa:
Mke wee mke gani, dini lini ulijua!
Alipozidisha kani, ndoaye nikajivua.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Wako mabwana wa shani, ningependa kunioa,
Hawamtii shetani, Mungu amewaongoa,
Nao wamomashakani, kwa mabibi walooa,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Tu wema hatujuani, wake na waume pia,
Twaingia mashakani, kwa wenzi waso murua,
Namlilia Manani, mume mwema kunioa,
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Nawe muombe, ndoa yenu kutulia,
Tusikuone mwakani, viragoumepania,
Mke na mume nyumbani, mumche Mola Jalia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Shairi hili limetungwa na Sheikh Amri Abedi.
 
Karibu tena Zonduma, naona umekua siku hizi!
 
Hili lilishawaikuletwa apa na mzee mwanakijiji....pitia huko jukwaa la lugha utapata majibu.
 
Du,kuna watu wenye mashairi huku, mi mpitaji tu
 
Shairi zuri, maneno mazuri pia!
 
Nafikiri "Mke asiye na mume" anafaa kumchumbia "Mume asiye na mke"
Angalizo: Hapo huyo mke asiye na mume anatakiwa kuwa makini na kutumia weledi mkubwa vinginevyo anaweza kuonekeana changudoa wakati akiwa ktk hizo harakazi zake .....
 
Zinduna naomba namba yako, napenda maneno yako naamini utakuwa mzuri pia.
 
Mke asiye na mume, akamchumbie nani?

Isingekuwa vigeni, mwanamke kuchumbia
Ningepita mitaani, mume kujitafutia,
Nisimuudhi Manani, ndio nimejizuia.
Mke asiye na mume akamchumbie nani?


Shairi hili limetungwa na Sheikh Amri Abedi.

Hivi atakuwaje MKE kama hana mume?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…