uvugizi
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,278
- 956
Moja ya ishara ya wewe kuelekea pabaya ni kuongezeka idadi ya marafiki ambao wanamawazo mabovu, hawana maono, hawajali kuhusu jamii,hawaheshimu wazazi au hawapendi kujifunza mambo ya kuwajenga , unakuta mtu mwaka mzima hajawahi kusoma hata kitabu kimoja kutokana na mazingira ya Maendeleo yake.
tabia yako ndiyo inayovuta hawa watu na kumbuka Mzoga ukianza kuoza kwenye uwazi fulani ataanza inzi mmoja atatua, jinsi mzoga unavyoendelea kuoza na kutoa harufu ndivyo inzi wanavyozidi kuongezeka ikiwa ni ishara kwamba huu mzoga umeoza kwelii.
Mzoga kuoza na kuwa na harufu mbaya ni Tabia zako ambazo zimevuta watu ambao sio sahihi (Inzi) na kama hutaki kuwa na tabia hiyo mapema fukia zile tabia ambazo ni mzoga wenye harufu mbaya na kuoza ili ubadilishe maisha yako.
Nionyeshe rafiki yako nikwambie tabia yako.
Be inspired.