NIPASHE: Interpol kuwasaka viongozi wachochezi wa dini

NIPASHE: Interpol kuwasaka viongozi wachochezi wa dini

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza sasa limeamua kutumia polisi wa kimataifa (Interpol) kuwasaka viongozi wawili wa dini wanaodaiwa kutorokea nchi za nje kukwepa kukamatwa kwa tuhuma za kurekodi kanda zenye maudhui ya uchochezi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa viongozi hao ni kati ya viongozi watatu waliokuwa wanasakwa na jeshi hilo tangu Februari mwaka huu kwa tuhuma za kufanya uchochezi.

Aliwataja viongozi wanaosakwa na Interpol kuwa ni Askofu wa kanisa la Tanzania Field Evangelism maarufu kama kanisa la ‘Kwa Neema’ anayedaiwa kutorokea nchini Marekani na Sheikh Irunga Hassan Kapungu, anayedaiwa kutorokea nchini India.

Hata hivyo alisema, Imam Hamza Omari ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi watatu wa dini wanaosakwa na jeshi hilo tayari amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kurekodi kanda za uchochezi wa kidini.

“Kama mnavyofahamu tangu Februari mwaka huu tulikuwa tukiwasaka viongozi hawa kwa tuhuma za kufanya uchochezi, lakini wakawa wametoroka. Tulifanikiwa kumkamata mmoja, wengine wakawa wametoroka, lakini tumepata taarifa kwamba mmoja yupo Marekani na mwingine yupo India, hivyo tumeamua kutumia Interpol kuwasaka na kuwatia mbaroni”alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Mangu, Sheikh Irunga Kapungu anatuhumiwa kurekodi kanda tatu tofauti zenye majina ya “Rudisha Heshima ya Uislaam, Bakwata ni tawi la Kanisa, na Mauaji ya Kinyama ya Sheikh Abood Logo wa Mombasa ambayo pia ndani yake kuna maudhui yanayoelezea unafiki katika Sensa.

Aidha, alisema kwamba Askofu Mpemba anadaiwa kurekodi kanda yenye jina la “Inuka Chinja Ule” huku Imam Hamza anadaiwa kurekodi kanda yenye jina la Ndege wote walie, akilia bundi uchuro”.

Kamanda huyo wa polisi mkoani Mwanza alisema kwamba kanda zote hizo zina maudhui yanayolenga kuchochea chuki kati ya dini moja dhidi ya nyingine na kati ya wananchi dhidi ya serikali yao.

Alisema kuwa mbali na kuwasaka watuhumiwa waliorekodi kanda hizo, jeshi la polisi pia limepiga marufuku usambazaji wake, na atakayebainika atakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uchochezi.

Alitoa wito kwa mtu yeyote mwenye kanda hizo kuzisalimisha polisi ifikapo Jumatatu ya Aprili 15, mwaka huu vinginevyo watakaokutwa nazo watahesabiwa kuwa wachochezi sawa sawa na waliozirekodi.


CHANZO: NIPASHE
 
Polisi acheni ujinga. Mnafikiri siku hizi kwa maendeleo ya kiteknolojia yaliyopo ujumbe unahitaji kanda ili usambae? Mbona mimi nimeweka kwenye simu yangu kama caller tune? Mbona naweza kuusambaza kwa njia ya mtandao kupitia youtube? Mbona naweza kuutuma kwa yeyote kama mms? Badilikeni jamani polisi japo hamjasoma lakini najua kuna wachache angalao wamepata kijielimu japo kidogo kwa nini msiwatumie?
 
Kisha sauti ikamjia kusema "Inuka Petro, uchinje ule".......Matendo ya Mitume 10:13

Sijasikia hiyo CD lakini kama ilikuwa inahimiza wakristo kuchinja (ama kuonyesha kutokuvunjwa kwa sheria wakichinja) itakuwa inachocheaje uvunjifu wa amani endapo hakuna sheria yenye kusema nani achinje?
Kama kuna sheria kwa nini wasiache ichukue mkondo waku insted serikali inataka kuwe na maridhiano baina ya dini mbili kuu?

Katika shule zote za kata nilizosoma sikupata kufundishwa kuwa kuchinja ni moja ya sababu za amani na utulivu wa nchi yetu.

Je, tuseme jeshi la polisi walitaka kubalance mwitikio wa jamii endapo wangekamata kiongozi kutoka dini moja????

Katika kukua kwangu tulikuwa tunamwita/peleka kuchinjiwa kitoweo kwa mzee Ramadhan.....hayo yalikuwa ni maamuzi ya familia ingawa tulikuwa hatulazimiki kama ambavyo hatulazimiki sasa!!!
 
Back
Top Bottom