Au kama una account na benki yako, waandikie mchanganuo wa mradi unaotaka kuufanya na uelezee huo mtaji wako ulionao. Ni matumaini yangu ya kwamba kama ni mradi wa millioni mbili na una hizo millioni 1.5 hawatakukatalia kukupa hiyo robo unayoihitaji. Kikubwa uwe mwumini wa benki ndiyo jambo kuu wanaloangalia. Na namna utakavyojieleza hasa kuhusu huo mradi na uoneshe mtirirko wa mapato unayotarajia kuyapata kutokana na huo mradi. Kila la kheri!