Nipe jina FM Radio

mwachalika

Member
Joined
Nov 24, 2009
Posts
32
Reaction score
15
Habari wadau wote jamvini. Radio mpya ya kisasa inategemewa kufunguliwa mkoani Tanga mwanzoni mwa 2015 hivyo tunaomba mawazo yenu kwenye jina la Radio. Tumeona ni vyema tukachanganya mawazo kwenye kutafuta jina la Radio hii. Yeyote atayetoa jina ambalo litaonekana linafaa kutumiwa na kituo hiki cha radio basi ataalikwa kuhudhuria ufunguzi na pia atabaki kwenye kumbukumbu ya kituo chetu. Mawazo yenu ni muhimu sana kwa wakati huu. Karibuni
 
redio inafunguliwa january 2015, halafu haina jina? heheheeh nadhani hamuwajui tcra. sisi tuna miaka 3 sasa tunasaka leseni. acheni kuleta utani humu
 
Ni radio ya vijana kupashana habari mbalimbali na entertainment. Ahsante sana kaka kwa swali zuri
 
Uuuuuwi jaman sijawahi ona hii,hiv tcra mnawajua au mnawasikia!!!! Ok ngoja tungoje hiyo januari na hapo hamna jina may b jan/2017
 
Mi naona muite jina la Amboni sijui ni fm au am.

sababu kuu za kuita Amboni,ni kuwa ilo jina la Amboni ni rahisi kupata umaarufu sababu watu wanajua amboni pia mtakuwa mnatangaza utalii wa Tanga hasa kwenye mapango ya amboni maana nilishaingia ndani umo yani ni maajabu tu .

Cha ajabu Amboni haitangazwi wakati kuna maajabu mengi sana.

Hivyo kwa uzoefu wangu niamini mkiita jina la Amboni radio mtakuwa maarufu sana wakat huo mtakuwa mmeisaidia Tanga kiutalii
 
Kuna baadhi ya watu wanaomba leseni wakiwa hawajanunua hata kifaa kimoja na hata eneo lenyewe la radio ni magumashi. Sisi tumejipanga vyema na kila kitu tayari mpaka setup ya jengo mzee
 
Kuna baadhi ya watu wanaomba leseni wakiwa hawajanunua hata kifaa kimoja na hata eneo lenyewe la radio ni magumashi. Sisi tumejipanga vyema na kila kitu tayari mpaka setup ya jengo mzee

tcra hawaamgalii majengo, kamati ya waziri haiangalii majengo fanyeni uchungizi kwa watu wengine. sisi tumenanza mwaka 2012 tukiwa na kila kitu na kibali tcra kilipita mapema ila mpaka navyokwambia hivi bado tunapigwa danadana tu. acha maneno ya kusikia
 
Ni kweli hatutaki kusikia ngoja na sisi tujionee wenyewe huo utaratibu wa TCRA. Shukrani kwa msaada
 
Ni kweli hatutaki kusikia ngoja na sisi tujionee wenyewe huo utaratibu wa TCRA. Shukrani kwa msaada

tz watu waajabu sana ndo maana nilihama. wabishi mpaka basi badala ya kufanya utafiti hahaha haya bana mpaka tcra wanakuja kwa inspection nadhani hata vifaa vitakuwa vimeoza au kuchakaa hahaha all de best
 
tz watu waajabu sana ndo maana nilihama. wabishi mpaka basi ya kufanya utafiti hahaha haya bana mpaka tcra wanakuja kwa inspection nadhani hata vifaa vitakuwa vimeoza au kuchakaa hahaha all de best

Ahhaah kaka umehama TZ? Pole sana, TZ ndio mambo yote ndugu. Tutabanana sana na TZ yetu
 
Iteni AMANI FM ikiwakilisha peace na milima ya amani ambayo ni kuna vivutio vingi vya utalii na ndio chanzo cha maji ambayo tunajivunia tanga. Nawashauri pia transmitter muweke mkanyagen ndo mtakuwa na coverage nzuri hadi handen kuliko kuweka tanga mjini
 

Ipeni Jina La ELECTION FM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…